Naibu Waziri, Ofisi ya Waziri Mkuu anayeshughulikia masuala ya Watu wenye Ulemavu Mhe. Ummy Nderiananga akizungumza na wanafunzi wa Chuo cha Ufundi Stadi cha Watu wenye Ulemavu Yombo wakati wa hafla ya chakula cha mchana siku ya Eid el fitr, Mei 14, 2021 Jijini Dar Es Salaam.
Sehemu ya Wanafunzi wa Chuo cha Ufundi Stadi cha Watu wenye Ulemavu Yombo wakimsikiliza Naibu Waziri, Ofisi ya Waziri Mkuu (Wenye Ulemavu) Mhe. Ummy Nderiananga (hayupo pichani) katika wa hafla ya chakula cha mchana siku ya Eid El Fitr iliyoandaliwa na Ofisi ya Waziri Mkuu.
Naibu Katibu Mkuu, Ofisi ya Waziri Mkuu Prof. Jamal Katundu akieleza jambo wakati wa hafla hiyo iliyofanyika katika Chuo cha Ufundi Stadi cha Watu wenye Ulemavu Yombo, Jijini Dar es Salaam.
Naibu Waziri, Ofisi ya Waziri Mkuu (Wenye Ulemavu) Mhe. Ummy Nderiananga (kulia) akijadiliana jambo na Naibu Katibu Mkuu wa Ofisi hiyo Prof. Jamal Katundu pamoja na Kaimu Mkuu wa Chuo cha Ufundi Stadi cha Watu wenye Ulemavu Yombo, Bi. Mariam Chelangwa (katikati) wakati wa hafla ya chakula cha mchana siku ya Eid El Fitr iliyoandaliwa na Ofisi ya Waziri Mkuu.
Naibu Waziri, Ofisi ya Waziri Mkuu (Wenye Ulemavu) Mhe. Ummy Nderiananga (wa pili kutoka kulia) akimpatia chakula Kassim Ally katika hafla ya chakula cha mchana siku ya Eid El Fitr iliyoandaliwa na Ofisi ya Waziri Mkuu.
Baadhi ya Wanafunzi wa Chuo cha Ufundi Stadi cha Watu wenye Ulemavu Yombo wakila chakula cha mchana katika sherehe ya Eid El Fitr Mei 14, 2021.
Naibu Waziri, Ofisi ya Waziri Mkuu (Wenye Ulemavu) Mhe. Ummy Nderiananga akifurahia jambo pamoja na Wanafunzi wa Chuo cha Ufundi Stadi cha Watu wenye Ulemavu Yombo wakila hafla ya chakula cha mchana iliyoandaliwa na Ofisi ya Waziri Mkuu katika sherehe ya Eid El Fitr Mei 14, 2021.
PICHA ZOTE NA OFISI YA WAZIRI MKUU
(SERA, BUNGE, URATIBU, KAZI, VIJANA, AJIRA NA WENYE ULEMAVU)
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...