MBUNGE wa Jimbo la  Mtama mkoani Lindi Nape Nnauye (CCM,)ameiomba Serikali kufanya marekebisho katika mfuko wa zao la korosho kwa kuurejesha kama ilivyokuwa awali pamoja na kurejeshwa kwa Sh.bilioni  55 kwa wakulima kutoka mfuko wa zao la korosho na kulipia pembejeo za kilimo ili kuendeleza zao hilo linalolingiza taifa fedha za kigeni.

Akizungumza leo Bungeni Jijini Dodoma wakati akichangia hotuba ya bajeti ya Wizara ya Kilimo 2021/2022 amesema, mwaka 2018  sheria ya tasnia ya korosho ilibadilishwa na kupelekea kufutwa kwa mfuko wa kuendeleza zao la korosho (Mfuko wa pembejeo,) ambao chanzo chake cha fedha ni tozo ya mauzo ya nje.

"Wakati marekebisho hayo yanafanyika Serikali ilihaidi kwamba inachukua fedha zilizokuwa zinapatikana na kupelekwa katika mfuko mkuu ili kuongeza ufanisi katika usimamizi na utarejeshwa kuendelea kusimamia zao hilo kama hapo awali,"amesema.

Nape amesema, imepita misimu mitatu tangu mabadiliko hayo yafanyike lakini fedha haijarudi katika zao hilo na baada ya fedha hizo kuchukuliwa uzalishaji wa zao la korosho ukashuka kutoka tani laki tatu na ishirini hadi laki mbili.

Aidha amesema kutorejeshwa kwa fedha hizo zilizokuwa  zikisimamia tafiti na kuendesha bodi ya korosho  wakulima wamebebeshwa mzigo huo kwa kukatwa shilingi 50 za kugharamia utafiti na kuendesha bodi ya korosho.

"Mbaya zaidi sasa kuna mapendekezo mengine ya kugharamia pembejeo kwa kumkata mkulima shilingi 110 kwa kilo kinyume na ahadi iliyotolewa ya kuwa tozo ya mauzo ya nje ingerudi kugharamia."

Ameongeza kwamba mwaka 2018 Sh.bilioni 37 iliingizwa katika mfuko huo na haikufanya kazi yoyote.

"Na hapa Serikali ilipata mapato ya zaidi ya shilingi trilioni moja, na mwaka huu uzalishaji umeshuka hadi kufikia tani laki mbili na 80 na tunahitaji bilioni 55  tulizohaidiwa katika zao hili," amesema.

Ameshauri kuundwa kwa bodi ya korosho iliyovunjwa miaka mitatu iliyopita, kuweka Mkurugenzi imara atakayeweza kuendesha bodi hiyo pamoja na kuwalipa wazalishaji wa miche ya korosho walioingia makubaliano na bodi na baadaye kutotambulika kwa kigezo cha kuwa watumishi wa Umma.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 1 mpaka sasa

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...