Na Zainab Nyamka, Michuzi TV 

RAIS Mstaafu wa Serially ya Awamu ya Pili Alhaj Ali Hassan Mwinyi ambaye pia ni Mkuu wa Chuo cha Afya na Sayansi Shirikishi ameongoza matembezi ya hisani kwa lengo la kuchangisha fedha ambazo zitasaidia wanafunzi wa chuo hicho zaidi ya 2000 kupatiwa chanjo ya Ini ili kujikinga na maambukizi ya ugonjwa huo.

Kwa mujibu wa Chuo hicho ni asilimia 2 tu ya wanafunzi 2600 ndio  wamefanikiwa kupata chanjo ya homa ya ini kutokana na changamoto ya kifedha na wengine kutokupata mkopo wa elimu ya juu.

 Akizungumza wakati wa uzinduzi wa matembezi hayo, Mwinyi amewataka madaktari kutimiza wajibu wao wanapokuwa mahala pa kazi ili kuokoa maisha ya watanzania na kutoa ushauri kwa wanafunzi wanaosoma udaktari katika chuo hicho. 

Matembezi hayo ya km 6 yakianza Masaki hadi Chuo cha MUHAS Muhimbili yaliweza kujumuisha viongozi mbalimbali akiwemo Naibu Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia Omary Kipanga, Mwenyekiti wa Baraza la Chuo Dkt Harrison Mwakyembe, Makamu Mkuu wa Chuo cha MUHAS  Profesa Andrea Pembe, wadau mbalimbali wa sekta ya afya, serikali ya wanafunzi MUHASSO na wanafunzi wa chuo hicho. 

Dkt Harrison Mwakyembe amesema elimu ya afya na tiba imekuwa inapanuka kwa kiasi kikubwa  na kupelekea  serikali kubeba mzigo mkubwa  wa gharama  kwani kwa sasa chuo kina wanafunzi takribani 4300 na wote wanatakiwa kupata chanjo ya homa ya ini ili kujikinga na maambukizi ya ugonjwa huo kwa sababu ya kukutana na watu mbalimbali pindi wanapotoa huduma. 

Amesema matembezi hayo yatakuwa ni endelevu kwani chanjo ya.homa ya ini ni muhimu sana  kwa wanafunzi wa udaktari, uuguzi, ufamaisia na meno na hiyo ni kulingana na mazingira wanayokutana nayo.

Aidha amesema gharama za kupata chanjo ya homa ya ini haipo katika bima ya afya na baada ya  wazo la kufanya matembezi ya hisani ni kuweza kuchangia kuletwa katika baraza la chuo lilipelekwa kwa Mkuu wa Chuo na kulipa baraka zote na wanawashukuru wadau waliojitolea kuchangia ikiwemo Wizara ya Elimu waliotoa milioni 7. 

Gharama za chanjo hiyo kwa mtu mmoja ni Sh.40,000 na kiasi kinachohitajika ni sh.Milioni 120 na Wanafunzi wanaosomea fani mbalimbali za udaktari, uuguzi, ufamasia, meno na zingine wanahitajika kupata chanjo ya homa ya ini kutokana na kukutana na watu mbalimbali wakati wa utoaji huduma.
Rais Mstaafu wa awamu ya Pili na Mkuu wa Chuo cha Afya na  Sayansi Shirikishi MUHAS Alhaj Ali Hassan Mwinyi akizungumza wakati wa uzinduzi wa matembezi ya hisani yaliyojulikana kama tembea nami yakihusisha uchangiaji wa fedha kwa ajili ya chanjo ya homa ya ini kwa wanafunzi wa chuo hicho.
Rais wa Awamu ya Pili na Mkuu wa Chuo cha Afya na Sayansi Shirikishi Muhimbili  MUHAS Alhaji Ali Hassan Mwinyi akikata utepe kuashiria uzinduzi wa matembezi ya hisani ya kuhamaisha uchangiaji wa fedha kwa ajili ya chanjo ya homa ya ini kwa wanafunzi wa Chuo cha Afya Muhimbili. Kulia ni Naibu Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia OMARY kipanga na Mwenyekiti wa Baraza la Chuo MUHAS Dkt Harrison Mwakyembe.
Rais wa Awamu ya Pili na Mkuu wa Chuo cha Afya na Sayansi Shirikishi Muhimbili MUHAS Alhaji Ali Hassan Mwinyi (wa tatu kushoto) akiwa katika matembezi ya hisani akiambatana na Naibu Waziri wa Elimu Omary Kipanga (wa pili kulia) Mwenyekiti wa Baraza la Chuo Dkt Harrison Mwakyembe (wa pili kushoto) na Makamu Mkuu wa Chuo Prof Andrea Pembe.
Wanafunzi na wadau mbalimbali wakiwa katika matembezi ya hisani ya kuchangia fedha kwa ajili ya chanjo ya homa ya ini kwa wanafunzi wa Chuo cha MUHAS

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...