Na Mwandishi wetu, Haydom


WANARIADHA 400 wametimua vumbi kwenye mashindano ya riadha ya Haydom Marathon  wilayani Mbulu Mkoani Manyara, lengo likiwa kujenga wodi ya watoto.

Mkurugenzi mtendaji wa tiba wa hospitali ya rufaa ya Haydom, Dkt. Paschal Mdoe, akizungumza mara baada ya mashindano hayo amesema watu mbalimbali wamejitokeza kushiriki mbio hizo.

Dkt. Mdoe amesema ujenzi rasmi wa wodi hiyo ya watoto unatarajia kuanza rasmi wakati wowote mwaka huu.

Mgeni rasmi wa michuano hiyo Naibu Waziri wa Tamisemi, David Silinde amesema atachangia  milioni 2 kwenye ujenzi wa wodi hiyo ya watoto.

"Pamoja na hayo mtanipatia karatasi ya orodha ya kuchangia ili niende nayo Bungeni tukasaidiwe kuchangia na kiasi cha pesa kitakachopatikana kitawasilishwa.," amesema Silinde.

Mkuu wa wilaya ya Mbulu, Dk Chelestino Mofuga amesema anaunga mkono ujenzi huo kwa kujitolea  milioni 1.

Mbunge wa Jimbo la Mbulu Vijijini, Flatei Maasay amesema amejitolea sh1.5 milioni kwa ajili ya kuchangia ujenzi wa wodi hiyo.

Katika mashindano ya kilomita 21 mwanariadha wa jeshi la wananchi, JWTZ, Joseph Panga alishika nafasi ya kwanza kwa wanaume na kujipatia sh500,000 na medali ya dhahabu.

Panga alifuatiwa na Josephat Gisemo wa Polisi aliyepata sh400,000 na medali ya fedha na watatu ni Shingade Giniki wa Katesh Wilayani Hanang' aliyepata sh300,000 na medali ya shaba.

Kwa upande wa wanawake, kilomita 21 Failuna Matanga wa Arusha alishika nafasi ya kwanza na kujipatia sh500,000 na medali ya dhahabu.

Grace Jackson wa JKT, alishika nafasi ya pili na kujipatia sh400,000 na medali ya fedha na watatu ni Angela John wa Arusha aliyepata sh300,000 na medali ya shaba.










Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...