Waziri wa Maliasili na Utalii, Dkt Damas Ndumbaro ametoa tahadhari kwa Wakazi wa Ruvuma kuwa  tembo zaidi ya 200 wapo nje ya Hifadhi Taifa ya Mwl.Nyerere kutokana na Wafugaji kuingiza makundi ya ng'ombe ndani ya Hifadhi hiyo.

Dkt. Ndumbaro  ametoa tahadhali hiyo hususani kwa wakazi wa wilaya  Tunduru na Namtumbo wakati alipotembelea vijiji sita vilivyoathiriwa zaidi na tembo ili kukutana na wananchi na kujibu kero mbalimbali zinazotokana na uvamizi wa tembo katika maeneo yao wakitokea Hifadhi ya Taifa ya Mwl.Nyerere.

Dkt.Ndumbaro amesema kuna  Watu wanasema tembo wameongezeka ndio maana kuna matukio ya tembo kuvamia mashamba na kujeruhi baadhi ya wananchi lakini takwimu zinaonesha tembo hawajaongezeka ila watu ndo wameongezeka.

"Miaka ya 80 tulikuwa na Tembo  takribani 134,000 na idadi ya Watanzania ilikuwa mil. 30 lakini hatukuwa na matatizo kama haya, Kwa sasa tuna tembo elfu 60 tu na idadi ya Watanzania imekuwa mil.60 , tujiulize akina nani wameongezeka, alihoji Dkt.Ndumbaro

Amesema Wenyeviti wa Vijiji wamekuwa wakiwakaribisha  Wafugaji na makundi ya ng'ombe na kisha kuingiza mifugo hiyo ndani ya Hifadhi hali inayowafanya tembo kutoka nje ya Hifadhi.

Amesema kwa mujibu wa utafiti wa Satelite uliofanyika hivi karibuni umeonesha tembo zaidi 200 wapo nje ya Hifadhi, Hivyo amewatahadharisha wananchi kutoa taarifa haraka pindi wanapoona makundi ya tembo yakiwa karibu kwenye makazi yao.

Amesema kufuatia ng'ombe hao kuingia ndani ya Hifadhi wamekuwa wakilazimika kutoka nje ya maeneo yao kwa sababu tembo hawapendi kuchangamana na ng'ombe kutokana na harufu ya madawa wanayotumia kuoshwa wakiwa katika majosho.

Kutokana na  hali hiyo, Waziri Dkt.Ndumbaro ameagiza  ng'ombe walioingizwa ndani ya Hifadhi watolewe haraka na wafugaji wenyewe  la sivyo ng'ombe hao wataifishwe na wasipouzika wapewe magereza kwa ajili ya chakula cha Wafungwa.


Aidha, Waziri Ndumbaro ametaja sababu nyingine iliyochangia Tembo hao  kutoka nje ya Hifadhi kuwa ni tabia ya baadhi ya Wananchi kulima kwenye kingo za Hifadhi hali inayowavutia tembo kutoka nje kwa ajili ya kula mazao hayo.

Amesema idadi ya mashamba kuathiriwa  pamoja na wananchi kujeruhiwa inazidi kuongezeka siku hadi siku si kwa sababu idadi ya tembo imeongezeka bali ni kutokana na idadi ya watu kuongezeka na kulazimika kufanya shughuli ndani ya Hifadhi.

Katika hatua nyingine, Dkt.Ndumbaro amewaonya Wananchi kuacha kulima katika Jumuiya ya  Hifadhi ya Wanyamapori kwa kuwa hali hiyo imechangia tembo kutoka nje ya Hifadhi kula mazao

Awali  akieleza kuhusu kero za wananchi wa jimbo lake la Namtumbo  Mhe. Vita Kawawa, amesema kuwa wananchi wa Jimbo lake la Namtumbo  kwa muda mrefu sasa wamekuwa wakiathiriwa na tembo wanaovamia makazi na mashamba yao na kumuomba  Waziri wa Maliasili na Utalii kuharakisha kulipa vifuta jasho na vifuta machozi kwa Wananchi waliopata adha zitokanazo na adha ya tembo.

Kwa upande wa Mbunge wa Tunduru Kaskazini, Hassan Kungu amemuomba Waziri wa Maliasili na Utalii, Dkt.Ndumbaro kuongeza fedha za vifuta jasho na vifuta machozi kwa sababu fedha wanayolipwa wananchi wake hailingani na thamani ya mashamba waliyoharibiwa na tembo

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...