Na Mwandishi wetu
CHAMA Cha Mapinduzi(CCM) kimempongeza Katibu Mkuu wa Chama hicho Daniel Chongolo kwa kuanza kutoa mwelekeo na dira ya majukumu ya sekretariet ya NEC kwa muktadha kuisimamia na kufuatilia utendaji wa Serikali utakoleta tija na manufaa kwa umma.
Hivyo sekreterieti ya NEC haitakuwa tayari kuona watanzania wakihangaika ,kutahabika na kukosa aidha haki za msingi, au wakifanyiwa dhuruma na udhalilishaji wa aina yoyote.
Hayo yamesemwa leo jijini Dar es Salaam na Katibu wa Itikadi na Uenezi wa Chama Cha Mapinduzi( CCM) Shaka Hamdu Shaka wakati akikabidhiwa ofisi rasm na aliyekuwa mtangulizi wake Humphrey Polepole.
Shaka amesema ni kawaida yanapotokea mabadiliko wahusika kukabidhiana kazi za kiofisi na kuongeza kama kazi ya utendaji za CCM , Katibu Mkuu Daniel Chongolo ni kama upele ulimpata mkunaji kutoka na upeo alionao kisiasa na kiutendaji
Amesema atakuwa tayari kutoa kila alichonacho kusaidiana na wenzake lakini pia atakuwa tayari kupokea na kujifunza kutoka kwa wenzake akichukua na kupokea mawazo, ushauri, miongozo na kuwa mjasiri wa kusimamia changamoto chini ya shabaha na malengo ya CCM
Aidha amezitaka taasisi za umma na za kiserikali kila moja kutimiza wajibu wake kwa kutumikia na kufuata miongozi ya kisera na malengo ya kimkakati yalioainishwa kwenye Ilani ya uchaguzi ya CCM ya mwaka 2015/2020.
"Wote ni mashahidi Rais Samia Suluhu Hassan amechukua jitihada za wazi za kujenga mahusiano yanayochochea msukumo wa biashara na uwekezaji,ameondoa vizuizi vya kibiashara kwa manufaa ya wote na amewahimiza wafanyabiashara na wananchi kulipa kodi,kodi isiwe bughudha na kizuizi bali kila mmoja alipe kwa wakati na hiari,"amesema Shaka.
Ameongeza Rais Samia ana nia ya dhati na kweli amedhamiria kujenga nchi huku akitaka iende kwa mwendo wa haraka ndio maana ameanza kufungua milango iliotaka kujifunga akifuata nyayo za watangulizi wake ambao wote walipikwa, kuandaliwa na kupewa dhamana uongozi na CCM.
"Kwa dhamana nilionayo naahidi kuwa kiungo na daraja kwa watendaji wenzangu na makundi ya wanahabari, wanamichezo, wasanii na walemavu .Rais samia ameshasema upepo uwe mwingi au kidogo jahazi litatia nanga katika bandari ya mafanikio. CCM pia inaunga mkono msimamo huo na kutekeleza kwa vitendo" amesisitiza .
Pia Shaka amewasihi viongozi wa taasisi za Serikali , mamlaka ,wakala mbalimbali za serikali na kujitafakari ili kuona muhimu qa kumuunga mkono Rais Samia kwa utendaju wenye tija hatimaye wananchi wanufaike na kufikia kilele cha maendeleo ya kiuchumi, kijamii na kisiasa .
Akizungumzia kukabidhiwa ofisi, Shaka amemshukuru Polepole kwa kazi aliyoifanya yeye na wenzake wote huku akiahidi kuacha wazi milango ya idara hiyo kwa namna yoyote ile ya kupokea ushauri kwa maslahi ya CCM na maendeleo Taifa
"Katibu Mkuu wetu amekusudia kuwa na Chama linachotegemewa na wananchi nyakati zote. CCM hakijawahi kuwa Chama cha masetla hivyo kitaendelea kubaki ni chama cha wakulima na wafanyakzi chenye nia ya kujenga jamii ilio sawa na huru,"amesema Shaka.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)








Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...