MAKAMU Mkuu wa Chuo Kikuu cha Mzumbe, Profesa Lughano Kusiluka, ameeleza mafanikio makubwa ambayo chuo hicho kimeyapata katika Awamu ya Tano na Sita ya Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.
Profesa Kusiluka amebainisha mafanikio hayo mbele ya Wahariri wa vyombo vya habari mbalimbali nchini kupitia Jukwaa la Wahariri Tanzania (TEF), waliotembelea Chuo Kikuu Mzumbe, Kampasi Kuu ya Morogoro na kupata fusra ya kutembelea maendeleo ya ujenzi wa miundombinu iliyokamilika.
Profesa Kusiluka amefafanua kuwa Chuo Kikuu cha Mzumbe kimewekeza zaidi ya Bil 13 kutokana na fedha zilizotolewa na Serikali, katika ujenzi wa vyumba vya madarasa na mabweni ya wanafunzi wa chuo hicho.
Amefahamisha kuwa ujenzi huo unalenga kukabiliana na changamoto ya upungufu wa vyumba vya madarasa ya kufundishia na mabweni ya kulala wanafunzi, ambao baadhi yao wanalazimika kutafuta makazi nje ya kampasi.
Vyumba vya kufundishia vilivyo katika miradi mipya ya miundombinu iliyokamilika ina uwezo wa kuhudumia wanafunzi 1,000 huku mabweni yakiwa na uwezo wa kutoa malazi kwa wanafunzi 1,024.
Aidha, amewashukuru Wahariri wa vyombo vya habari kwa kutenga muda wao kutembelea Chuo Kikuu cha Mzumbe, chuo ambacho kinajivunia mafanikio makubwa ikiwa ni pamoja na kuzalisha viongozi wengi ndani Serikali akiwemo Rais wa Awamu ya Sita Mhe. Samia Suluhu Hassan.
Aidha Profesa Kusiluka amebanisha kuwa Vyombo vya Habari, Wahariri na Waandishi wa habari wana umuhimu mkubwa wa kuhabarisha, kuelimisha na kuburudisha jamii ikiwa ni pamoja na kuchochea maendeleo.
Wakizungumza baada ya kutembelea
majengo yaliyokamilika (Vyumba vya madarasa na mabweni ya wanafunzi), wahariri
hao wamepongeza mafaniko makubwa yaliyotokana na dhamira ya Serikali ya
kuwekeza kwenye Sekta ya elimu ili kutoa fursa kwa Watanzania wengi zaidi
kunufaika na Elimu nchini.




Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...