Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Amos Makala akizungumza na viongozi wa dini Mkoa wa Dar es Salaam kuhusiana na masuala mbalimbali ya Mkoa.

Mkuu wa  Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania (KKKT) Dayosisi ya Pwani na Mashariki  Dkt.Alex Malasusa akichangia katika kikao Cha viongozi wa dini kilichoitiwa na mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam.


Mjumbe wa Halmashauri ya Kuu ya Baraza Kuu la Waislaam Shekh Hamis Mataka akizungumza katika kikao cha viongozi wa dini kilichoitishwa na Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam.
Katibu wa Kamati ya Amani ya Mkoa wa Dar es Salaam Alhad Mussa Salum akizungumza kuhusiana na Kamati hiyo inavyofanya kazi kwa ushirikiano katika masuala ya dini wakati wa Kikao cha Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam na viongozi dini kilichofanyika Ukumbi wa Anatoglo jijini Dar es Salaam.


Na  Chalila Kibuda,Michuzi TV 

MKUU wa Mkoa wa Dar es Salaam Amos Makalla amesema kuwa wamachinga watawekewa utaratibu mazingira  mzuri wa kufanya biashara na usio utaratibu uliokuwepo wa kupanga biashara zao mbele ya maduka.

Mkuu wa Mkoa huyo ameyasema hayo wakati alipokutana na viongozi wa dini ambao walimwambia kuhusiana na wamachinga kupanga vitu katika barabara za watembea kwa miguu na kulazimika kupita katikati ya barabara.

Amesema kuwa Ana makakati wa kampeni ya Usafi ambapo viongozi wa dini ni muhimu kuubiri kwa waumini wao na kuweza kufanikiwa kwa kampeni hiyo.

Makala amesema kuwa anategemea kupata ushirikiano kwa viongozi wa dini wa Mkoa wa Dar es Salaam.

Hata hivyo suala la amani katika Mkoa wa dini viongozi wa dini wanaweza kuzungumza na waumini pamoja kuombea watu kuacha ujambazi na ukabaji.

Aidha amesema kuwa kunaweza  kukawa na waumini na watoaji wa sadaka na michango mingi kanisani na msikitini lakini nyuma fedha hizo zinatokokana na ujambazi au uuzaji wa dawa za kulevya.

Mkuu wa Kanisa la KKKT Dayosisi ya Pwana na Mashariki Dkt. Alex Malasusa amesema kuwa sadaka ya mtu jambazi au muuza dawa za kulevya ni chukizo mbele ya Mungu.

Amesema kuwa watatoa ushirikiano kwa mkuu wa Mkoa kuhakikisha anatimiza majukumu yake ikiwemo kumuombea.

Mjumbe wa Halmashauri Kuu la Baraza Kuu la Waislaam Tanzania (Bakwata) Sheikh Hamis Mataka amesema kuwa kushughulikia wauzaji Unga wasiangalie kiivuli cha watumiaji bali ni kuangalia mti unaofanya kuwepo kwa kivuli hicho ambao ni waingizaji  wa dawa hizo.

Katibu wa Kamati ya Amani Mkoa wa Dar es Salaam Sheikh Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Alhad  Mussa Salum amesema Kamati ya Amani imefanya kazi nyingi pamoja na kutatua migogoro ya ndani ya dini zote.

Amesema kuwa watatoa ushirikiano kwa Mkoa wa Dar es Salaam kama walivyotoa kwa watangulizi waliopita.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...