
VIJANA wanaojishugulisha na kilimo hai kwenye wilaya ya Chamwino mkoa wa Dodoma wameiomba serikali iwasaidie kupata uhakika wa masoko ya mazao yao ikiwemo alizeti, mahindi, kunde, ufuta na mazao ya mboga mboga.
Wamaetoa
ombi hilo jana Jumamosi (01.05.2021) wakati wataalam wa Wizara ya Kilimo
wanaofanya ufuatiliaji wa utekelezaji wa Mkakati wa Taifa Vijana kushiriki kwenye sekta ya Kilimo
(NYSA) kuzalisha ajira walipotembelea
vikundi sita vya vijana.
“Tunalima
mboga mboga mboga pia alizeti hapa kijijini lakini changamoto yetu imekuwa
uhaba wa masoko ya mazao yetu hali inayopunguza morali ya vijana kuendelea na
kazi za Kilimo” alisema Christopher Joseph kijana mjasiliamali.
Akizungumzia
kuhusu kazi zilizofanywa na shirika la Kilimo Endelevu (SAT) linalotekeleza
mradi wa Wanawake Dodoma katika Maendeleo ya Kilimo na Biashara (DWABI) Mratibu
wake Elizabet Kilia alisema jumla ya vijana 2,563 kati yao wasichana 2,354 na
wavulana 209 wamefikiwa na kuunganishwa kwenye vikundi vya kilimo hai (organic
farming.)
Aliongeza
kusema jumla ya vikundi 90 katika wilaya za Chamwino, Mpwapwa na Dodoma
wamefikiwa na elimu ya kilimo hai na ujasiliamali kupitia shirika la SAT ambapo
linalenga kuboresha maisha ya vijana hususan akina mama wadogo (young mothers)
kiuchumi kupitia kilimo ambao wamezaa mapema wakiwa na umri mdogo .
Elizabet alisema kwa upande wa ujasiliamali jumla ya
vijana 1,900 wamejengewa uwezo kwenye ujasiliamali kwa nadharia na vitendo
kuweza kutengeneza bidhaa za kijasiliamali kama batiki, kuongeza thanani ya
zao la ubuyu, sabuni za maji na mikoba ya shanga.
Naye
Mratibu wa Mkakati wa Vijana Kushiriki katika Kilimo toka Wizara ya Kilimo
aliyeongoza tumu ya wataalam kukagua miradi ya Vijana Revelian Ngaiza aliwapongeza
vijana wa Chamwino kwa ubunifu wao uliokuza uzalishaji wa mazao hali ilisaidia
kubaidilisha maisha yao kwa kuwa na uhakika wa kipato kwenye kaya.
Ngaiza
aliongeza kusema suala la uhaba wa masoko kwa mazao ya kilimo ni agenda kuu ya
serikali ya awamu ya sita ambapo mikakati imewekwa ili kuwezesha wakulima
wapate masoko na kuuza mazao yao, hivyo amewataka vijana kutokata tamaa bali
waendelee kujishughuli kazi za kilimo ikiwemo za uongezaji thamani mazao ya
kilimo na mifugo.
“Rais
Samia Suluhu Hassan tayari ameshatoa maagizo kwa wizara ya Kilimo na ile ya
Viwanda na Biashara kuhakikisha mazao ya wakulima yanapata masoko ya uhakika. Agizo hilo alilotoa wakati akihutubua Bunge huvu karibuni, hivyo vijana
endeleeni kulima kwa kuzingatia tija na soko litapatikana” alisisitiza Ngaiza.
Kuhusu
changamoto ya vijana kupata ardhi na kuondokana na gharama kubwa ya kukodi
Ngaiza alitoa wito kwa Halmashauri nchini kote kutenga ardhi maalum kwa ajili
ya vijana kwenye vijiji ili waweze kuzalisha mazao ya Kilimo na kuwa na uhakika
wa ajira na kipato hatua itakayosaidia utekelezaji wa mkakati wa Taifa kuhusu
vijana kushiriki kwenye sekta ya Kilimo.
Kwa
upande wake Mkurugenzi wa shirika la Kilimo Endelevu (SAT) Janet Maro alisema
wapo tayari kununua mazao yote ya vijana yaliyozalishwa kwa njia ya Kilimo hai
msimu huu ikiwemo alizeti, karanga, ufuta, mahindi na mpunga.
Katika
kuhakikisha vijana wanawezeshwa na kusimamiwa kuzalisha mazao kwa njia ya
Kilimo hai SAT tayari imefanikiwa kutoa mafunzo kwa maafisa ugani 40 toka wilaya
za Chamwino (19),Dodoma (1) na Mpwapwa (20) mafunzo yaliyotolewa kwenye kituo
cha mafunzo Vianzi mkoani Morogoro mwaka 2020.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...