Na Mwaandishi Wetu Mtwara

WANANCHI wa kata ya Mkoreha Wilani Tandahimba wameeleza kufurahishwa namna ambavyo Benki ya NMB Kanda ya Kusini inavyojitoa katika kusaidia upatikanaji wa huduma za jamii kwa wananchi mkoani Mtwara.

Wakizungumza katika hafla ya kukabidhiwa madawati 50 yaliyotolewa na Benki hiyo, Tawi la Tandahimba kwa shule ya msingi Msifuni Tandahimba, wananchi hao wamesema NMB imekuwa mstari wa mbele katika kutoa misaada mbalimbali kusaidia jamii hizo kimaendeleo.

“NMB ndio baba lao hapa kwetu Mtwara, ni benki ya kipee kwa kweli katika kutusaidia sisi wananchi haswa kwenye huduma za muhimu kama vile shule, mahospitalini, Benki hiyo iko mstari wa mbele kutusaidia pale tunapowaitaji na wakati mwingine wanakuja bila sisi kuwaomba,” amesema Mwenyekiti wa Shule ya msingi ya Msifuni Jafari Chimela.

Amesema licha ya benki hiyo kupeleka madawati hayo 50 kwa shule ya Msifuni, NMB imekuwa ikipeleka misaada kama vile mabati ya kuwezekea madarasa ya shule mbalimbali, na hospital, vitanda vya wagonjwa vikiwemo vitanda maalumu vya kujifungulia akina mama, mashuka, kujenga maghala na kutoa misaada ya chakula na malazi pindi inapotokea majanga katika Mkoa wa Mtwara.

Jafari amesema msaada wa madawaiti umekuja baada ya kamati ya shule na chama cha msingi cha kata ya Msifuni kupeleka ombi kwa benki hiyo kuwaomba wawasaidia madawati kwa ajili ya wanafunzi wa shule za msingi Msifuni na Magome ambazo zilikuwa na uhitaji mkubwa wa madawati.

“Tulienda tukawaelezea kuhusu mahitaji ya madawati katika shule zetu na wao bila kusita wakaomba kututembelea shule hizo mbili kuona hilo tatizo na wakaahidi kutuletea madawati na kweli leo wametimiza ahada yao na kwa haraka sana,” amesema.

Diwani wa Kata ya Msifuni Maajabu Mnungu amewaomba wananchi wa Kata yake na Mtwara kutumia benki ya NMB katika kuweka pesa zao ili kuendelea kuipa nguvu benki hiyo katika kuwasaidia.

“Mimi ombi langu ni moja tu kwenu wananchi wenzangu, tuitumie benki yetu ya NMB katika kuweka hela zetu haswa sisi wakulima, benki yetu ni benki ambayo kwanza inatujali sana bila kuangalia sura zetu inapotokea shida wanatukimbilia na kutusaidia na tunapowahitaji wanakuja haraka, ili waendelee kutusaida lazima tutumie benki yao katika kupata huduma za fedha,” amesema.

Akipokea madawati hao kutoka kwa Meneja wa Kanda ya NMB Janet Shango, Mkuu wa Wilaya ya Tandahimba Sebastian Waryumba amesema NMB ni wadau wakubwa wa maendeleo ya Tandahimba huku akiwaomba waendelee na moyo huo huo wa kusaidia.

“NMB ni benki ya kipekee sana katika kujitolea kwa wananchi, kwa Tandahimba wamekuwa wadau wakubwa wa maendeleo, nawaomba waendelee na moyo huo huo,” amesema na kuongeza kuwa NMB wameonyesha mfano mzuri sana kwa kusaidia wananchi kwa kile wanachokipata.

DC huyo ameunga mkono viongozi wa kata kuwa wananchi kuwaunga mkono NMB kwa kutumia benki hiyo katika huduma za fedha ili kwa kuwa kile wanachokipata kutokana na huduma zao za kifedha wanakileta kwa wananchi kwa ajili ya kusaidia maendeleo ya wananchi.

Amewataka kamati ya shule ya Msifuni na uongozi wa shule kutunza madawati hayo ili yaweze kuduma kwa maufaa ya wanafunzi wengi hapo shule.

Kwa upande wake, Meneja wa NMB Kanda ya Kusini Janet Shango amesema benki ni jukumu la benki hiyo kusaidia wananchi kimaendelea kwa sababu wateja wao wengi ni miongoni mwa wananchi ambao pia wananufaika na misaada hiyo inayotolewa na benki hiyo.

Mkuu wa Wilaya ya Tandahimba Sebastian Waryumba (Kushoto) akikabidhi madawati hayo Kwa Diwani wa Kata ya Mkoreha Wilayani Tandahimba Maajabu Mnungu Kwa ajili ya shule ya msingi ya Msifuni.
Mkuu wa Wilaya ya Tandahimba (aliyekaa kushoto) akiwa kwenye picha na pamoja na Meneja wa NMB Kanda ya Kusini Janet Shango (aliyekaa kulia) wakiwa kwenye picha ya pamoja na Viongozi wa Kata na mara baada ya kupokea madawati 50 Kwa ajili ya shule ya msingi ya Msifuni


Wanafunzi wa shule ya msingi ya Msifuni iliyopo Kata ya Mkohera Wilayani Tandahimba wakitoa burudan katika hafla ya kukabidhiwa madawati 50 yaliyotolewa na Benki ya NMB Tawi la Tandahimba Kwa shule hiyo.



Sehem ya wananchi waliojitokeza katika hafla ya kukabidhiwa madawati kwa ajili ya wanafunzi wa shule ya Msingi Msifuni Wilaya ya Tandahimba
Mkuu wa Wilaya Sebastian Waryumba na Meneja wa Benki ya NMB Kanda ya Kusini wakiwa kwenye picha ya pamoja na wanafunzi wa shule ya msingi ya Msifuni huku wakifurahia mara baada ya kupokeaa madawati 50 kutoka Kwa NMB Tawi la Tandahimba.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...