MWANAHARAKATI huru David Gaudance Msuya amewashauri wanawake kumuunga mkono Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Rais Samia Suluhu Hassan katika utekelezaji wa majukumu yake ikiwa ni pamoja na kumuombea kwa Mungu.

Akizungumza na waandishi wa habari leo Ilala jijini Dar es Msuya amesema, akiwa mwanaharakati huru atasimama na Rais Samia mwanamke wa kwanza kuliongoza taifa, jasiri na msikivu ambaye ameanza kazi vizuri na kwa weledi.

Amesema, wanawake kote nchini waoneshe ushirikiano na kumwombea kwa Mungu apate afya njema katika utekelezaji wa majukumu ya kitaifa na watanzania kwa pamoja waoneshe ushirikiano kwa kuungana na kudumisha tunu za Taifa.

"Tumuache Mama afanye kazi, kuweka maneno mtandaoni ni udhaifu na kuonesha kushindwa, Tuzidi kuliombea Taifa letu amani izidi kutawala na mafanikio tuliyoanza kuyaona kwa Mama Samia yaendelee na kudumu." Amesema.

Pia amewashauri watanzania kuwaombea viongozi waliopo madarakani na waliostaafu na kuacha tabia ya kuzusha taarifa zisizo za kweli kupitia mitandao ya kijamii.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...