WIZARA ya Mambo ya Ndani ya Nchi Idara ya Uhamiaji imewasimamisha kazi wafanyakazi wake watatu kutokana na  tukio la askari wa Uhamiaji kutumia nguvu dhidi ya Alex Raphael Kyai kama video fupi ilivyoonekana katika mitandao ya kijamii.

Akizungumza na wandishi wa habari  leo Mei 30, 2021 Kamishina Jenerali wa Uhamiaji  Dkt Anna Makakala amesema Mei 27 mwaka 2021, Idara ya Uhamiaji ilimkamata mtuhumiwa wa utapeli  anayefahamika KWa jina Alex Raphael Kyai katika Ofisi ya Uhamiaji Kurasini, Dar es salaam ambaye aliongozana na mteja wa huduma za pasipoti, aliyemtambulisha kama mkewe.

Aidha Dkt.Makakala  amesema baada ya mahojiano, ilibainika kuwa mtuhumiwa huyo amekuwa na tabia ya kuwalaghai na kupokea fedha kutoka kwa wateja mbalimbali ili waweze kupata pasipoti kwa haraka, pia mtuhumiwa huyo amekuwa akijitambulisha kama Mtumishi wa Taasisi nyeti ikiwemo Taasisi ya Kuzuia na kupambana na Rushwa (TAKUKURU).

" Idara ya Uhamiaji inakiri kutokea kwa tukio hilo na pia inalaani kitendo kilichofanywa na askari wa Uhamiaji kwa kutumia nguvu kinyume cha sheria na maadili ya kazi zao, hata hivyo Idara ya Uhamiaji tayari imechukua hatua za kinidhamu dhidi ya askari hao" Dkt.Makakala.

Idara ya uhamiaji inatoa wito kwa wananchi wote wanaohitaji huduma za kiuhamiaji kufika wenyewe katika ofisi za Uhamiaji, pia Uhamiaji wanawahakikishia kwamba idara itaendelea kutoa huduma zake kwa weled, uwazi na bila kutumia mtu wa kati ( Vishoka) Na Idara hiyo ya Uhamiaji inaomba kupata ushirikiano KUTOKA kwa wananchi kwa kutoa taarifa za watu wanaofanya vitendo vya aina hiyo.

Aidha Idara ya uhamiaji imetoa onyo kwa yeyote ambaye atajaribu kujifanya kuwa Afisa wa Uhamiaji au Afisa wa Serikali ili kumsaidia mtu mwingine kwa maslahi yake binafsi hatua kali dhidi yake zitachukuliwa kwa mujibu wa Sheria.

Kamishina Jenerali wa Uhamiaji  Dkt Anna Makakala 

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...