Mtendaji Mkuu wa Shirikisho la Vyama vya Ushirika Tanzania(TFC) Florian Haule akizungumza leo Mei 26 jijini Dar es Salaam kuhusu Maadhimisho ya Siku ya  vyama vya ushirika duniani ambayo yanatarajiwa kufanyika Julai 3 mwaka huu na kitaifa yatafanyika Tabora.
Mtendaji Mkuu wa Shirikisho la Vyama vya Ushirika Tanzania(TFC) Florian Haule akifafanua jambo kwa waandishi wa habari kuhusu mafanikio na changamoto za vyama vya ushirika nchini.
Florian Haule ambaye ni Mtendaji Mkuu wa Shirikisho la Vyama vya Ushirika Tanzania akisiliza maswali kutoka kwa mwandishi wa habari(hawapo pichani) wakati wa mkutano huo.

Said Mwishehe, Michuzi TV
SHIRIKISHO la Vyama vya Ushirika Tanzania(TFC) limesema kuwa kuanzia Juni 23 hadi Julai 3 mwaka huu watakuwa wakiadhimisha Siku ya Ushirika Duniani na wanatarajia katika kilele cha maadhimisho hayo Waziri Mkuu Kassim Majaliwa atakuwa mgeni rasmi.

Kwa mujibu wa Shirikisho hilo, maadhimisho hayo kwa Tanzania yatakuwa yakifanyika kwa mara 20 wakati kwa duniani yatakuwa yakiadhimishwa kwa mara ya 99, na hivyo kila mwaka jamii ya wanaushirika hujumuika na wanajamii wengine na wadau wa ushirika kusherehekea siku hiyo.

Akizungumza leo Mei 26,2021 jijini Dar es Salaam, Mtendaji Mkuu wa Shirikisho la Vyama vya Ushirika Tanzania(TFC) Florian Haule amesisitiza Waziri Mkuu Kassim Majaliwa ndio anatarajiwa kuwa mgeni rasmi na katika maadhimisho hayo kutakuwa na shughuli mbalimbali ambazo zitafanywa na vyama hivyo vya ushirika.

Amesema miongoni mwa shughuli ambazo ziatafanyika kutakuwa na maonesho lakini kutakuwa na uchangiaji damu utakaofanywa na wana ushirika na mwaka huu kitaifa yatafanyika Viwanja vya Nane Nane mkoani Tabora.

"Shughuli zitakazofayika kutakuwa na maonesho ya bidhaa na huduma za vyama na wadau , kongamano la wanaushirika na wadau wake, shindano la isha ya wanafunzi wa shule ya msingi, sekondari na vyuo vikuu, kutoa damu kwa wahitaji, kupanda miti ili kuhifadhi mazingira.

"Pia kutakuwa na kutoa misaada mbalimbali katika vituo vya afya na hospitali , kupata huduma za afya kutoka kwa madaktari bingwa watakaopiga kambi katika viwanja vya maonesho.Aidha kutakuwa na burudani kutoka kwa wasanii mbalimbali nchini."Amesema Haule.

Aidha amesema kauli mbiu kwenye maadhimisho hayo itakuwa inasema "Ushirika tujijenge upya kwa ubora na tija" huku akifafanua kauli mbiu hiyo imekuja kutokana na changamoto ya janga la Corona ambayo dunia imepitia.Hivyo tumeona tusimame na tujijenge upya."

Akielezea zaidi maadhimisho hayo, Haule amesema pia kutakuwa na uzinduzi wa tuzo maalum kwa viongozi mbalimbali ambao wametoa mchango wao kwa kiasi kikubwa katika vyama vya ushirika nchini.

Akizungumzia kwa kifupi kuhusu muelekeo wa ushirika, Haule amesema Serikali ya Awamu ya Sita inajipanga kuipandisha nchi yetu iweze kufikia kuwa nchi yenye uchumi wa kati kupitia uendelezwaji wa sekta ya viwanda na nyinginezo.

"Mazingira hayo yanatosha kueleza mwelekeo ushirika wa vyama vya ushirika vitajipanga pamoja na vyama vya ushirika kushiriki katika ujenzi wa uchumi wa viwanda.Aidha vyama vya ushirika vinatarajiwa kuwa chombo cha uzalishaji wa malighafi za viwandani na nyinginezo.

"Kuwa sekta itakayotoa ajira nyingi zaidi , sekta yenye kuchangia sehemu kubwa ya pato la Taifa,kuwa sekta ya kuvutia kundi la vijana na kujiunga katika ushirika,"amesema Haule.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...