Waziri wa Maliasili na Utalii, Dkt.Damas Ndumbaro aahidi kutumia ushawishi wake kuwahamasisha Mawaziri wenzake pamoja wa watu kawaida kujifunza mchezo wa gofu kufuatia ombi la Balozi wa Ufaransa nchini Tanzania, Mhe.Frederic Clavier kufanya hivyo

Ametoa kauli hiyo jana wakati wa hafla ya kutoa zawadi kwa Mabalozi na Wataalamu wa nchi mbalimbali ambao ni Wachezaji na Wanachama wa Chama wa gofu nchini kufuatia kumalizika kwa mashindano ya Gofu yaliyoandaliwa na Balozi wa Ufaransa nchini Tanzania yaliyofanyika Mwezi April mwaka huu Jijini Dar es Salaam.

Hafla hiyo ya utoaji zawadi kwa Wachezaji wa gofu imefanyika nyumbani kwa Balozi huyo, Mhe.Frederic Clavier na kuhudhuriwa na Mabalozi na Wataalamu mbalimbali wanaoziwakilisha nchi zao nchini Tanzania ambao ni Wachezaji wa Gofu na Wanachama wa Gofu nchini Tanzania.

Amesema kufuatia ombi la Balozi wa Ufaransa nchini Tanzania, Mhe.Frederic Clavier mbali ya kuwahasisha Mawaziri pia atawahamasisha Wabunge kujifunza mchezo huo ili kuwa timu bora ya Bunge ya mchezo wa gofu hali itakayopelekea Wabunge hao kuendeleza mchezo huo katika majimbo waliyotoka.

Akizungumza katika hafla hiyo, Waziri Dkt.Ndumbaro amewapongeza Washiriki hao na kuwaaahidi kuendeleza mchezo huo kwa kuunganisha na utalii wa michezo ili kuhamasisha Mabalozi hao kutembelea vivutio vya Utalii vilivyopo nchini.

‘” Nawaahidi kuandaa mashindano mengi zaidi ya Gofu ambayo nitawashirikisha karibu vivutio vya Utalii ili mkishacheza gofu mbajipumzisha kwa kuwa tembo na simba” alisema Ndumbaro

Kwa upande wake Balozi wa Ufaransa nchini Tanzania, Mhe. Frederic Clavier ametoa wito kwa Watanzania kujifunza mchezo wa gofu huo kwani ni mchezo kama michezo mingine

Amewatoa hofu Watanzania kuwa mchezo huo haubagui ni wa watu wote wenye kipato cha chini na cha juu na sio mchezo wa Watu wa Matajiri na Wasomi pekee

Amesema gofu ni mchezo rahisi sana kujifunza na sio mchezo mgumu, ” Jitokezeni kujifunza mchezo wa Gofu ni ajira na pia ni burudani kama ulivyo mchezo wa mpira wa miguu” alisema Mhe.Balozi Frederic Clavier

Katika hatua nyingine amempongeza Waziri Dkt. Ndumbaro kwa kuwa Mwanachama pekee wa Mchezo wa Gofu kati ya Mawaziri wote nchini Tanzania na hivyo kutoa wito kwa Mawaziri wengine kucheza mchezo huo.
Waziri wa Maliasili na Utalii, Dkt.Damas Ndumbaro akizungumza na Balozi wa Ufaransa nchini Tanzania, Mhe.Frederic Clavier wakati wa hafla ya utoaji zawadi kwa Wachezaji wa gofu kufuatia mashindano ya mchezo wa Gofu yaliyomalizika ambayo yaliandaliwa na Balozi wa Ufaransa nchini Tanzania, Mhe. Frederic Clavier iliyofanyika jana nyumbani kwake Balozi Jijini Dar es Salaam na kuhudhuriwa na Mabalozi na Wataalamu mbalimbali wanaoziwakilisha nchi zao nchini Tanzania ambao ni Wachezaji wa Gofu na Wanachama wa Gofu nchini Tanzania.
Balozi wa Ufaransa nchini Tanzania, Mhe.Frederic Clavier akiwa mke wake akizungumza kabla ya kumkaribisha Waziri wa Maliasili na Utalii, Dkt. Damas Ndumbaro kufungua hafla ya utoaji zawadi kwa Wachezaji wa mashindano ya gofu yaliyaondaliwa na Balozi huyo katika hafla iliyofanyika nyumbani kwake Balozi Jijini Dar es Salaam na kuhudhuriwa na Mabalozi na Wataalamu mbalimbali wanaoziwakilisha nchi zao nchini Tanzania ambao ni Wachezaji wa Gofu na Wanachama wa Gofu nchini Tanzania ambapo Balozi huyo ametoa wito kwa Watanzania kujifunza mchezo wa gofu. Kushoto ni mke wake wa Balozi.
Waziri wa Maliasili na Utalii, Dkt.Damas Ndumbaro (kulia) akikabidhiwa cheti cha ushiriki wa mashindano ya gofu yaliyoandaliwa na Balozi wa Ufaransa nchini Tanzania, Mhe.Frederic Clavier wakati wa hafla ya utoaji zawadi kwa Wachezaji wa gofu iliyofanyika nyumbani kwake Balozi Jijini Dar es Salaam na kuhudhuriwa na Mabalozi na Wataalamu mbalimbali wanaoziwakilisha nchi zao nchini Tanzania ambao ni Wachezaji wa Gofu na Wanachama wa Gofu nchini Tanzania.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...