Raisa Said,Pangani.

SHUGHULI za ulinzi wa rasilimali za  bahari Wilayani hapa zinatarajiwa kuimarika zaidi baada ofisi ya Kikundi  cha Ulinzi Shirikishi  Beach - Management Unit (BMU) Kipumbwi Wilayani Pangani Mkoani Tanga kuzinduliwa na mwenge wa Uhuru

Ofisi hiyo ya kisasa imezinduliwa na kiongozi wa mbio za Mwenge Maalum wa uhuru  Kitaifa mwaka 2021 Josephine Mwambashi baada ya kakamilika kwa asilimia 98.

Akizungumza kuhusu  mradi huo  unaotekelezwa  na  Wizara  ya Mifugo na Uvuvi  Sekta ya  Uvuvi kupitia  Mradi  wa SWIOfish Tanzania  Bara  unafadhiliwa na Banki ya Dunia Mwambashi alisema ni matarajio kuwa shughuli za ulinzi zitaimarika.

Akisoma taarifa baada ya Mwenge wa uhuru kufika katika Ofisi hiyo  Kaimu Afisa Mifugo na Uvuvi  Aristariki Kimario Alisema kuwa mradi huo ulioanza kutekelezwa July 28 mwaka jana ulitakiwa kukamilika  Desemba  3 mwaka jana  nakwamba umegharimu sh. Million 151.5  ikiwa ni pamoja na ongezeko la thamani.

Alisema kuwa mradi huo  utaimarisha  usimamizi  wa rasilimali za Uvuvi kwa kujenga  miundombinu, kusogeza zaidi  usimamizi  wa rasilimali ngazi  ya Jamii yani BMU ,kuimarisha  mahusiano  Kati ya wavuvi , serikali na jamii ambayo inasimamia  shughuli za uvuvi na  kusogeza  huduma ya wagani kwa kuwapatia  sehemu nzuri ya kufanyia kazi  na kusimamia rasilimali za uvuvi kwa ujumla.

Hata hivyo alisema kuwa katika kuhakikisha  ubora wa kazi unazingatiwa  viwango na vigezo uhakiki wa mara kwa  Mara wa ubora  wa viwango ,mazingira na usalama kazini ulifanyika.

Waziri wa Maji  ambaye ni Mbunge wa Jimbo hilo Jumaa Aweso alisema wao kama pangani  hawakujaliwa kupata dhahabu lakini wamejaliwa kuwa na bahari ambapo aliongeza kuwa wanaishukuru  serikali kwa kuwapatia fedha kwa ajili ya ujenzi wa jengo hilo la ofisi kwa ajili ya BMU.

Aweso alisema licha ya kukamilika kwa jengo hilo lakini halina samani za ndani hivyo aliwataka wakae pamoja ili waangalie namna ya kupata samani hizo za ofisi

Hata hivyo Kiongozi wa mbio za Mwenge kitaifa alisema kuwa ameridhishwa na ujenzi huo nakwamba ubora wa jengo unaendana na thamani gharama halisi za mradi huo.




Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...