Na Gift Thadey, Simanjiro
WATU 165 wamejitokeza kupima maambukizoli ya Virusi vya ukimwi katika mkesha wa mbio maalum za mwenge wa uhuru kwa mwaka 2021 kwenye Wilaya ya Simanjiro Mkoani Manyara.
Mkuu wa Wilaya ya Simanjiro, mhandisi Zephania Chaula ameyasema hayo Mji mdogo wa Orkesumet baada ya mwenge kuhitimisha mbio zake wilayani Simanjiro.
Amesema kati ya watu hao 165 waliopima VVU kwenye mkesha huo wa mwenge, wanaume walikuwa 112 na wanawake waliojitokeza ni 53.
Amesema baada ya kupima na kutolewa majibu imebainika kuwa watu watatu ambao ni wanaume wameathirika sawa na asilimia 1.8 ya waliopima kwenye mkesha huo.
Pia, amesema watu 11 ndiyo waliojitokeza kujitolea damu wakiwemo wanaume tisa na wanawake watatu huku watu 76 wakipima malaria.
Kiongozi wa mbio za mwenge wa uhuru, Luteni Josephine Mwambashi, amesema jamii inapaswa kuendelea kuchukua tahadhari ya maambukizi ya VVU.
Luteni Mwambashi amesema mbio maalum za mwenge wa uhuru kwa mwaka huu pia umekuwa ukitoa ujumbe wa kujikinga na maambukizi ya VVU katika maeneo mbalimbali wanapopita.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...