WAZIRI wa Maji Jumaa Aweso ametembelea na kukagua Mtambo wa kusukuma maji (Pump Station No.03) eneo la Maweni Arumeru. Mtambo huo ni miongoni mwa mitambo mitano ya kusukuma maji inayojengwa kwa ajili ya kupeleka maji katika Jiji la Arusha na viunga vyake. 

Kukamilika kwa ujenzi wa mitambo hiyo kutawezesha kuongezeka kwa uzalishaji na usambazaji wa maji katika Jiji la Arusha ambapo mahitaji ya sasa ya maji ni lita milioni 104 na uzalishaji wa sasa ni lita milioni 64. 

Ukamilifu wa mradi huu mkubwa wa maji utamaliza kabisa tatizo la upatikanaji wa huduma ya majisafi na salama kwa wakazi wa Arusha na viunga vyake.




Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...