WAZIRI wa Maji  Jumaa Aweso (Mb) amehitimisha  ziara ya kikazi mkoani Arusha kwa kukagua ujenzi wa miundombinu ya mradi wa maji katika Kijiji cha Ligamba, wilayani Arumeru.

Akiwa katika kikao na  madiwani wa eneo hilo jana usiku baada ya ratiba ndefu ya mchana alifanya maamuzi ya kukamilisha mradi huo ambao kwa sasa umefika asilimia 80 ya utekelezaji wake.

Katika kikao hicho pamoja na mambo mengine Waziri Aweso alitumia nafasi hiyo kuzungumza moja kwa moja na Katibu Mkuu wa Wizara ya Maji, Mhandisi Anthony Sanga kwa njia ya simu na kufikia muafaka kuwa sehemu iliyobaki ya ujenzi imalizike ili wananchi waanze kupata huduma ya maji.

Mradi huu unasimamiwa na Wakala wa Usambazaji Maji Vijijini (RUWASA) na  utanufaisha zaidi ya wakazi 6,244 wa vjiji  vitatu ambavyo ni Likamba, Oleitushura na Nengungu.


Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...