KATIKA kuunga mkono kampeni inayoongozwa na taasisi ya VOYOTA na wadau wengine katika kuchangisha taulo za kike, FLAVIANA MATATA FOUNDATION iliyopo jijini Dar Es Salaam imetoa boksi kumi na mbili na nusu(12.5) zenye jumla ya taulo za kike 300 kwa taasisi ya vijana ya VOYOTA kwa niaba ya wanafunzi wa kike wa shule ya sekondari ya Mgeta iliyopo Mkoani Morogoro.

Akikabidhi pads hizo, mwakilishi wa FLAVIANA MATATA FOUNDATION, Kisha Lushaju alisema, kuwa taulo hizo za kike zitawanufaisha mabinti 25 wanaotoka katika familia zenye hali duni.

"Tunatoa taulo hizi za kike ili ziweze kuwanufaisha mabinti 25 wanaotoka kwenye hali duni, waweze kujisitiri mwaka mzima wanapokuwa kwenye hedhi." Alisema Kisha.

Akipokea pads hizo kwa niaba ya taasisi ya vijana ya VOYOTA, Naamala Samson ambaye pia ni mkurugenzi wa LaKisha Solutions, aliishukuru FLAVIANA MATATA FOUNDATION kwa msaada huo wa pedi za LAVY. 

Pia aliongezea kuwa, "Taulo hizi zitasaidia sana wasichana hawa kuwa katika hali ya usafi na kujiamini wawapo shuleni na tunawaomba wadau wengine kujitokeza kuunga mkono kampeni hii inayolenga kufikia mabinti 500".

Taulo hizi za kike za LAVY zitapelekwa mkoani Morogoro kwenye shule ya sekondari ya Mgeta. Kampeni hii itaisha ifikapo mwishoni mwa mwezi wa sita mwaka huu.

Kwa atakayependa kuwasilisha mchango wa fedha au taulo za kike, anakaribishwa kwa kuwasiliana na waratibu-VOYOTA 0755 427 000
Mwakilishi wa FLAVIANA MATATA FOUNDATION, Kisha akimkabidhi
mkurugenzi wa LaKisha Solutions, Naamala Samson boksi za pedi kutoka FLAVIANA MATATA FOUNDATION.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...