Mkuu wa Jeshi la Polisi nchini IGP Simon Sirro, amesema kufuatia Operesheni ya wiki moja iliyofanyika katika Jiji la Dar es salaam, wamefanikiwa kukamata silaha za moto pamoja na wahalifu waliokuwa wakijihusisha katika matukio mbalimbali ya kihalifu.
IGP Sirro amesema hayo leo wakati wa kikao kazi cha kufanya tathmini, mafanikio na changamoto ambapo pia ameelekeza kufanyika kwa operesheni ya mwezi mmoja kwa nchi nzima ili kubaini mianya ya uhalifu na wahalifu.
Aidha, IGP Sirro amewaelekeza Makamanda wa Polisi nchini kufanya
operesheni ya usalama barabarani dhidi ya magari yote yasiyokidhi vigezo vya
kuwepo barabarani ili kuwahakikishia usalama watumiaji wa vyombo vya
moto.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...