Hyasinta Kissima-Afisa Habari

Halmashauri ya Mji Njombe

Mbunge wa Jimbo la Njombe Mjini Deo Mwanyika leo amekabidhi gari ya kubebea wagonjwa yenye thamani ya shilingi milioni 200 katika kituo kipya cha Afya Kifanya, vyanzo vikuu vya ujenzi wa kituo hicho ikiwa ni mapato ya ndani ya Halmashauri na Nguvu za Wananchi ambapo Wananchi wa Kata ya Kifanya walichangia kiasi cha Shilingi millioni thelathini na nane na laki saba na Halmashauri kupitia mapato ya ndani iliweza kutoa kiasi cha shilingi milioni mia tatu hamsini.

Akiwasilisha taarifa ya ujenzi wa Kituo hicho Mtendaji wa Kijiji cha Kifanya Barick Kabelege amesema kuwa lengo la ujenzi wa Kituo hicho linatokana na utekelezaji wa Ilani ya Chama Cha Mapinduzi kwa kuhakikisha kuwa katika kila Kata inatakiwa kuwa na Kituo cha Afya na dhumuni la pili ikiwa ni kutokana na ongezeko la idadi ya watu wanaohitaji huduma za Kiafya katika Zahanati ya sasa ya Muungano ongezeko lililosababishwa na uwepo wa shamba la chai Mahoro na Unilever, shughuli za kibiashara na umbali wa takribani Kilomita 60 kutoka ilipo Hospitali ya Mji Kibena.

“Mpaka sasa tumefanikiwa kujenga majengo 6 ya kiwemo jengo la upasuaji, mortuary, jengo la kufulia jengo la mama na mtoto, maabara na miozi. Tunao pia wachangiaji mbalimbali ambao wamechangia katika kufanikisha ujenzi huu Hayati Dkt. John Pombe Magufuli alituchangia milioni 10, Mbunge aliyepita alichangia mifuko 100 ya saruji, Mheshimiwa Diwani mifuko 50 ya saruji, Umoja wa Wanawake CCM Wilaya ya Njombe mifuko ya saruji 20, Taasisi ta Kifedha Kifanya kiasi cha shilingi laki saba na nusu na CCM Wilaya mifuko 10 ya saruji ambapo kwa pamoja tumekamilisha majengo hayo.”

Akizungumza wakati wa hafla ya makabidhiano hayo Mbunge wa Jimbo hilo Deo Mwanyika amewashukuru Wananchi wa Kifanya kwa kuitikia wito wa Serikali na kuunga mkono jitihada za Serikali katika kuimarisha Sekta ya Afya katika jimbo hilo jambo lililopelekea Halmashauri hiyo kuwa kati ya Halmasahuri 20 pekee zilizofanikiwa kupata magari hayo nchi nzima.

“Ombi lenu limekua ndio msingi wa ushindi wetu.Ujenzi wa kituo cha afya kifanya ni jambo la kutukuka.Naomba niwahakikishieni kuwa mchango wangu ni kuhakikisha kuwa kituo hiki kinafunguliwa na vifaa tiba vinapatikana. Kwa leo nitawachangia mifuko 100 ya saruji ila yaliyosalia nitakwenda kuyatekelza kwa nguvu zote.Tunamshukuru pia Rais wetu Samia Suluhu Hassani kwani kwa uongozi wake Njombe tutafanya makubwa”Alisema Mwanyika

Aliendelea kusema.”Niwaombe twende tukalitunze gari hili na pia tuhakikishe kuwa tunaitambua na kuilinda mipaka ya kituo chetu ili kuepusha migogoro”Alisema

Kwa upande wake Mwenyekiti wa CCM Wilaya ya Njombe Edward Mgaya amewapongeza Wananchi hao na kuwataka kuendeleza utamaduni wa kuchangia kwani licha ya kupatiwa gari lakini kuna wakati mwingine magari hayo yanashindwa kutoa huduma kutokana na kukosekana kwa fedha za mafuta na matengenezo na kuwataka Wabnanchi kuendelea kulihudumia gari hilo ili Wananchi waendelee kupata huduma za msingi

Atilio Mwapinga na Leah Mkalawa wote wakazi wa Kifanya wanasema kuwa wanaishukuru Serikali kwa kupatia gari hilo kwani kwa sasa walikua wanategemea gari kutoka kituo cha afya mjini takribani kilomita 60 kama akitokea mgonjwa wa rufaa jambo ambalo lilikuwa lilikua linahatarisha maisha ya watu hususani wanawake wajawazito. Mpaka sasa kituo hicho kipo katika hatua za umaliziaji huku kiasi cha Shilingi milioni mia mbili ishirini na tano kikitarajiwa kutumika kukamilisha ujenzi huo ambapo Mkurugenzi wa Halmashauri ya Mji Njombe Illuminatha Mwenda amewahakikishia Wananchi kukamilisha hatua hiyo.

Diwani wa Kata ya Makowo Honoratus Mgaya akiwaongoza waimbaji wakati wa hafla ya kukabidhi gari ya kubebea wagonjwa katika kituo cha Afya Kifanya

Mbunge wa jimbo la Njombe Mjini Deo Mwanyika wakicheza kwa furaha mara baada ya kukabidhi gari ya kubebea wagonjwa kwa Wananchi  katika kituo cha afya Kifanya

Mbunge wa jimbo la Njombe Mjini Deo Mwanyikaakikata utepe kuashiria kuanza rasmi kwa huduma za kubebea wagonjwa katika Kitupo cha Afya Kifanya

Mbunge wa jimbo la Njombe Mjini Deo Mwanyika (mwenye kofia)akihoji jambo wakati akipokea taarifa ya ujenzi wa jengo la mama na mtoto katika kituo cha afya Kifanya kutoka kwa Mganga Mkuu wa Halmashauri Dkt. Yesaya Mwasubila (mwenye karatasi) wakati wa hafla ya kukabidhi gari ya wagonjwa katika kituo hicho

 

Picha ya pamoja ya waheshimiwa madiwani wa Halmashauri ya Mji Njombe wakiwa pamoja na mbunge wa jimbo hilo mara baada ya  makabidhiano ya gari hilo

Wananchi wakishangilia na kufurahia kupatiwa gari ya kubebea wagonjwa
Diwani wa Kata ya Kifanya akitabasamu mara baada ya kuingia ndani ya gari hiyo
 

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...