Na Leylah Nassib - DSJ

BAADA ya purukushani za hapa na pale hatimaye msanii maarufu wa Filamu  Frida Kajala Masanja maarufu kama Kajala pamoja na mwanaye Paula kupitia kurasa zao za mtandao wa Instagram wameeleza ujio wa kitu kipya mjini  'Mom & daughter like Twins reality show' ambapo Kajala amewataka watu wakae kwa kupoa kideoni kusubiria  Reality Show hiyo itakayoanza hivi karibuni.

 Kupitia mtandao huo kajala ameandika kuwa  kila kitu kitakuwepo kwenye Show hiyo ambayo ni maisha yao halisi kiujumla yeye na mwanaye pamoja na watu ambao wanawahusu katika maisha yao  wataonekana pia. 

Ni life style ya ambayo wawili hao wameamua kushiriki na watanzania kupitia TV huku  mwongozaji  wa kipindi hicho ni Director maarufu  Lamata Leah ambaye pia kupitia ukurasa wake wa Instagram  amewahakikishia mashabiki wake ubora wa kipindi hicho na kusema kuwa watu wanamjua vizuri hivyo hawezi kuwaangusha katika jambo hilo, hivyo watu wakae mkao wa kula kusubiri ni nini kitajiri katika show hio ya Mama na mwana.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...