AFISA Utawala wa kampuni ya ujenzi ya Makame Mwinyi Generals Supplies, Batuli Bakari (39) na fundi umeme Said Abdallah (33), wamefikishwa katika mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu wakikabiliwa na shtaka la kusafirisha dawa za kulevya.

Katika hati ya mashtaka iliyosomwa mahakamani hapo na wakili wa serikali Yusuph Abood mbele ya Hakimu Mkazi Mkuu Rita Tarimo imedai kuwa Mei 5, 2021 huko Mikocheni katika manispaa y Kinondoni jijini Dar es s Salaam washtakiwa walikutwa wakisafirisha gramu 194.93 za dawa za kulevya aina ya Heroine Hydrochloride.

Hata hivyo washtakiwa hawakuruhusiwa kujibu kitu chochote mahakamani hapo kwa kuwa mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu haina mamlaka ya kusikiliza kesi za dawa za kulevya.

Kesi hiyo imeahirishwa hadi Juni 17, 2021 kwa ajili ya kutajwa kwa mujibu wa upande wa mashtaka upelelezi katika kesi hiyo bado haujakamilika.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...