KWA sababu ya kujali afya na usalama, sasa Mashahidi wa Yehova watakusanyika pamoja kwa njia ya video badala ya kukutana pamoja uso kwa uso katika viwanja vya michezo na maonyesho, kumbi za mikutano na kwenye maeneo yao ya Ibada kama walivyofanya hapo awali kabla ya janga. Mwaka huu itakuwa mara ya pili kukusanyika kwa njia hiyo baada ya makusanyiko ya uso kwa uso 6,000 hivi katika nchi 240 kufutwa.

Kwa zaidi ya miaka 50, Mashahidi wa Yehova wamekuwa wakikutana katika miji yote nchini Tanzania ili kufanya makusanyiko ambayo ni sehemu kuu ya matukio yao ya kila mwaka. Katika mwaka wa 2020, janga lilivuruga desturi yao ya kukutana pamoja bila kutarajiwa na hivyo kusababisha uamuzi wa kufutilia mbali makusanyiko yanayofanywa uso kwa uso/ana kwa ana ulimwenguni pote na kuanzisha matukio yanayofanywa kote duniani kwa njia ya video. Hiyo ilikuwa mara ya kwanza kwa Mashahidi wa Yehova, ambao wamefanya makusanyiko ya umma katika viwanja vya michezo na maonyesho, kumbi za mikutano na kwenye maeneo yao ya Ibada duniani kote kuanzia mwaka wa 1897.

Kichwa cha Kusanyiko la mwaka huu wa 2021 ni “Uwe Mwenye Nguvu kwa Imani!”. Kusanyiko hilo litafanywa katika kila familia au mtu mmoja mmoja ulimwenguni pote katika lugha zaidi ya 500 kwa miisho juma sita katika miezi ya Julai na Agosti 2021, na hivyo kuwaunganisha watu milioni 15-20 katika nchi 240. Kwa kuwa kusanyiko hilo hufanywa Ijumaa hadi Jumapili, programu hiyo itapatikana katika sehemu sita, yaani vipindi vya asubuhi na alasiri. Sehemu ya kipindi cha “Ijumaa” itapatikana kwa ajili ya kutazamwa moja kwa moja katika tovuti yetu kupitia intaneti au kupakuliwa kuanzia Juni 28, 2021.

Kwa kuwa mikusanyiko ya watu wengi inachochea maambukizi, kwa hekima Mashahidi wa Yehova wameamua kufanya matukio haya kwa njia ya video kwa mwaka wa pili mfululizo. Kwa kupendeza, badiliko hili halijapunguza msisimko wa tukio hilo la kila mwaka. Mashahidi wa Yehova ulimwenguni pote wanawaalika watu wote wajiunge nao katika tukio hili la kihistoria. “Imani imewasaidia ndugu zetu ulimwenguni pote waendelee kusonga mbele hata katika janga,” alisema Zadok Mwaipwisi, Msemaji wa Mashahidi wa Yehova. “Imani yetu itaendelea kutuunganisha katika ibada – hata kwa njia ya video – huku mamilioni wakikutanika katika nyumba zao ulimwenguni pote ili kufurahia programu ya kiroho yenye kuimarisha na kuchochea.”

Watu wote wanakaribishwa wahudhurie tukio hili kwa kutembelea tovuti yetu, JW.ORG katika mtandao au JW Broadcasting kwenye programu za JW Library iOS au Android zinazopatikana bila malipo, au kwa mifumo ya kutazama moja kwa moja kwenye intaneti kama vile kupitia ROKU TV, Apple TV, na mingineyo. Programu hiyo inapatikana bila malipo na kila mtu anaweza kuipata. Ratiba iliyo hapa chini ndiyo itakayofuatwa ulimwenguni pote ili kupakua na kutazama moja kwa moja kwa kutumia intaneti.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...