Na Karama Kenyunko Michuzi TV
MAHAKAMA ya Hakimu Mkazi Kisuru imeelezwa kuwa, mazungumzo ya makubaliano (Plea bargaining) ya kumaliza kesi ya uhujumu uchumi inayomkabili Mkurugenzi wa Kampuni ya Kufua Umeme (IPTL), Herbinder Seth yanasuburi Muongozo wa Mkurugenzi mpya wa Mashtaka (DPP).
Wakili wa serikali Mwandamizi Wankyo Simon ameeleza hayo leo Juni 3, 2021 mbele ya Hakimu Mkazi Mkuu, Huruma Shaidi wakati kesi hiyo ilipokuja kwa ajili ya kutajwa na kujua hatma ya mazungumzo hayo na upelelezi ulipofikia.
"Mheshimwa Hakimu, kesi leo imekuja kwa ajili ya kutajwa, upelelezi bado na pia mazunguzo ya kumaliza kesi dhidi ya mshtakiwa Seth yanaendelea pale yalipoishia, Qtunasuburi muongozo kutoka kwa DPP mpya aliyeteuliwa hivi karibuni na Rais wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan ili tuweze kuwakilisha hapa mahakamani.
Awali Seth na Makandege waliwasilisha ombi kwa DPP wakionesha nia yao ya kutaka maliza kesi kwa kukiri makosa yao lakini, Mei 6, 2021 Wakili Makandege aliondoa nia yake ya kufanya makubaliano na DPP akieleza kwamba mazungumzo hayo hayana afya na yamechukua muda mrefu kukamilika.
Mbali na Seth washtakiwa wengine Katika kesi hiyo ni mfanyabiashara James Rugemalira na wakili Joseph Makandege
Rugemarila, ambaye ni Mkurugenzi wa VIP na mmiliki mwenza wa zamani wa IPTL na Sethi ambaye ni Mwenyekiti Mtendaji wa PAP, wanadaiwa kutenda makosa hayo katika Jiji la Dar es Salaam na nchi za Afrika Kusini, Kenya na India.
Washtakiwa wanakabiliwa na mashtaka 12 yakiwemo ya utakatishaji fedha, miongoni mwa mashtaka hayo yapo ya kula njama, kujihusisha mtandao wa uhalifu, kughushi na kutoa nyaraka za kughushi na kujipatia fedha kwa njia ya udanganyifu, kutakatisha fedha na kusababisha hasara ya Dola za Marekani 22,198,544.60 na Sh 309,461,300,158.27.
Washtakiwa wanadaiwa kati ya Oktoba 18 ,2011 na Machi 19, 2014 jiji Dar es Salaam walikula njama katika nchi za Afrika Kusini, Kenya na India ya kujipatia fedha kwa njia ya udanganyifu.
Mwanasheria Makandege, anakabiliwa na mashtaka matano likiwemo la kuisababishia Serikali hasara ya Dola za Marekani 980,000.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...