Mkurugenzi wa Mawasiliano na Jamii DAWASA Neli Msuya akizungumza na watendaji mbalimbali wa serikali, wenyeviti wa serikali za mitaa wakati wa kikao cha kujadili Mradi wa Usafi wa Mazingira unaosimamiwa na Mamlaka ya Majisafi na Usafi wa Mazingira Dar es Salaam DAWASA uliofanyika leo Jijini Dar es Salaam.
Watendaji mbalimbali wakiwa makini kusikiliza mada zinazowasilishwa wakati wa kikao hicho.
Meneja Usafi wa Mazingira nje ya Mtandao Mhandisi Charles Makoye akizungumza na watendaji mbalimbali wa serikali, wenyeviti wa serikali za mitaa wakati wa kikao cha kujadili Mradi wa Usafi wa Mazingira unaosimamiwa na Mamlaka ya Majisafi na Usafi wa Mazingira Dar es Salaam DAWASA uliofanyika leo Jijini Dar es Salaam.
 


Na Zainab Nyamka, Michuzi Tv

MAMLAKA ya Majisafi na Usafi wa Mazingira Dar es Salaam DAWASA imeanza kutekeleza mradi wa usafi wa Mazingira kwa Wilaya zote ili kuondoa changamoto ya utiririshaji wa majitaka kwa maeneo yaliyopembezoni mwa Mji.

Mradi huo unaotokelezwa na DAWASA unatarajia kukamilika mwaka 2023 na utahusisha maeneo ambayo hayajapimwa.

Akizungumza na watendaji mbalimbali, Mkurugenzi wa Mawasiliano na Jamii DAWASA Neli Msuya amesema wamekutana na viongozi mbalimbali wakiwemo watendaji wa Kata, wenyeviti wa serikali za mitaa, madiwani, wasimamizi wa afya na maendeleo ili kujadili kwa pamoja mradi mkubwa wa usafi wa mazingira unaoenda kutekelezwa katika maeneo yao.

Msuya amesema, mradi huu unatekelezwa na Serikali kupitia Dawasa na kufadhiliwa na Benki ya Dunia  na utaenda kuondoa changamoto zote za utiridishaji wa majitaka katika maeneo yaliyopembezoni mwa mji kwa kujenga mitambo ya uchakataji majitaka karibu na maeneo hayo.

Amesema, kuna mifumo mingi ya kimkakati ambapo Dawasa watajenga mitambo ya uchakataji majitaka na kuongeza wigo ya unyonyaji wa maji hayo kwa kusogeza karibu huduma hiyo kwa jamii na gharama nafuu.

"Sera ya serikali ni kuboresha huduma za mazingira katika jamii, asilimia 80 ya maji yaliyotumika yanakuwa ni majitaka na jukumu la Dawasa ni kulinda na kutunza mazingira,"amesema Msuya.

Kwa upande wa wawakilishi wa Wananchi Diwani wa Kata ya Azimio kutoka Halmashauri ya Manispaa ya Temeke Amina Ismail amesema mradi huu ni mzuri na unaenda katika maeneo yaliyo na changamoto hiyo.

Amina amesema, changamoto kubwa katika maeneo hayo ni miundombinu inayosababisha magari yakunyonyea majitaka yasifike lakini ni muhimu Dawasa kufika kwenye maeneo hayo na kuwapa elimu wananchi ili iwafikie kwa ukubwa zaidi.

Dawasa inatekeleza mradi huo ndani ya mkoa wa Dar es Salaam na utajenga mtambo mkubwa wa uchakataji wa majitaka katika maeneo ya Buguruni, Mbezi Beach na Kurasini.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...