MWANZILISHI mwenza wa Taasisi ya Wanasayansi Chipukizi Young Scientists Tanzania  (YST), Dk Gozibert Kamugisha amesema kwa sasa wanafunzi wengi wameona masomo ya sayansi kama fursa, hivyo wamekuwa wakichangamkia masomo ya sayansi ikilinganishwa na miaka 10 iliyopita.

Amesema huko nyuma ilikuwa nadra kukuta wanafunzi wa kike wakisoma masomo ya mchepuo wa sayansi lakini sasa hivi ni tofauti, wapo wengi wanasoma masomo hayo.

Akizungumza na Michuzi  jijini Dar es Salaam ,Dk.Kamugisha amesisitiza kwamba kwa sasa hali limebadilika baada ya kuwapo mwamko mkubwa kwa wanafunzi wa kike kusoma masomo hayo,hivyo ametoa shukrani kwa Serikali, wadau,wasa na walimu kwa kutoa hamasakwa mabinti wa Tanzania.

Dk Kamugisha amesema Shirikisho la YST limefanya kazi ya kuamsha chachu ya kisayansi kwa wanafunzi wa shule za sekondari kupitia kuhamasisha wanafunzi kufanya tafiti na kugundua vitu vinavyoisaidia jamii.

Ameongeza kuwa zamani mwalimu alikuwa akifundisha kwa kutumia vitabu yaani anafundisha sayansi kwa chaki ubaoni, kwa sasa walimu wanatumia njia za vitendo na wanafunzi wanaelewa zaidi na kuyapenda masomo ya sayansi.

 Dk.Kamugisha.katika kuhakikisha masomo ya sayansi yanaendelea kupendwa,  ndiyo sababu ya maonyesho ya wanasayansi chipukizi ya mwaka huu kupata washiriki wengi kutoka mikoa yote Tanzania.

"Idadi ya wanafunzi wanaotaka kushiriki maonnyesho ya wanasayansi chipukizi imeongezeka kutoka maombi 604 mwaka jana hadi maombi zaidi ya 670 mwaka huu. Maonesho ya wanasayansi chipukizi yatafanyika Oktoba mwaka huu yakijumuisha kazi za kisayansi 150,"amesema.

Dk Kamugisha amesema, mwaka jana walipokea maombi yenye miradi ya kisayansi 604 ambayo ilichuujwa na kubakisha miradi 123 iliyochuana kitaifa. Mwaka huu, YST imepokea zaidi ya maombi 670 inayojumisha wasichana na wavulana ambayo imechuujwa kupata miradi 579.

“Yalikuja maombi ya miradi zaidi ya 670 tumeyachuuja kupata miradi 579 ambayo wanafunzi wamefundishwa kuboresha mawazo yao,” amesema Dk Kamugisha na kuongeza kwamba  mtazamo wa watoto wa kike kuhusu ugumu wa masomo ya sayansi nao unabadilika taratibu.

"Jambo linaloonyesha siku zijazo kutakuwa na wanawake wengi katika masomo hayo muhimu kwa katika ukuaji wa uchumi kupitia sayansi na teknolojia."

Kwa upande wake Mwenyekiti wa Taasisi ya KJF inayodhamini maonyesho hayo, Yusuph Karimjee amesema inatia hamasa kuona sayansi siyo jambo gumu miongoni mwa wanafunzi na wakati wanaanza kudhamini maonyesho ya wanasayansi, ni shule nne pekee ndiyo zilijitolea kufanya maonyesho hayo.

Hivyo  kwa sasa kufikia hatua ya maonyesho hayo kufanyika kimkoa katika mikoa 25 inatia moyo.“Wanafunzi walioshiriki katika kila mwaka programu za YST wameendelea na kuwa madaktari, wauguzi, wahandisi na wafamasia. Kila mmoja hufanya tofauti  na kuchangia katika maendeleo ya uchumi,” amesema.Mwanzilishi mwenza wa Taasisi ya Wanasayansi Chipukizi Young Scientists Tanzania (YST) Dr Gozibert Kamugisha (katikati) akizungumza na waandishi wa habari (hawapo pichani) leo  jijini Dar es Salaam kuhusu maonesho ya wanasayansi chipukizi yatakayofanyika mwezi Oktoba mwaka huu yatakayojumuisha kazi za kisayansi zipatazo 150. Maonesho hayo yatatanguliwa na maonesho yatakayofanyika kwenye mikoa 25 ambapo zaidi ya kazi za kisayansi 300 zitaoneshwa na wanasayansi. Wapili kutoka kushoto ni Makamu wa Rais na Mwenyekiti wa kampuni ya Shell Tanzania, wa pili kutoka kulia ni Mwenyekiti wa Taasisi ya Karimjee Jivanjee Foundation (KJF) Yusuph Karimjee.   
Mwanzilishi mwenza wa Taasisi ya Wanasayansi Chipukizi Young Scientists Tanzania (YST) Dr Gozibert Kamugisha (kushoto) akiteta jambo na Mwenyekiti wa Taasisi ya Karimjee Jivanjee Foundation (KJF) Yusuph Karimjee leo jijini Dar esalaam.
Mwanzilishi mwenza wa Taasisi ya Wanasayansi Chipukizi Young Scientists Tanzania (YST) Dr Gozibert Kamugisha (kulia) akitetajambo na Makamu wa Rais na Mwenyekiti wa kampuni ya Shell Tanzania,Jared Kuehl leo jijini Dar es Salaam.
(Picha na Emmanuel Masssaka wa Mchuzi Tv)

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...