Charles James, Michuzi TV


WABUNGE wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania wameombwa kuunga mkono hoja ya kuwepo kwa maadhimisho ya siku ya mwanamke mwenye ulemavu.

Kauli hiyo imetolewa na Naibu Spika wa Bunge, Dk Tulia Ackson kwenye mkutano wa pamoja wa wadau wa Walemavu na Wabunge ulioandaliwa na Taasisi ya Ikupa Trust jijini Dodoma.

Akizungumza katika mkutano huo, Dk Tulia amewaomba Wabunge hao kuiunga mkono hoja hiyo pindi itakapoletwa bungeni na Mbunge wa Viti Maalum Stella Ikupa.

Naibu Spika Amesema uwepo wa siku ya mwanamke mwenye ulemavu itasaidia kuongeza wigo wa kujadili changamoto na matatizo wanayokumbana nayo wanawake wenye ulemavu nchini.

Dk Tulia amesema uwepo wa siku hiyo utatoa nafasi kubwa ya kujadili nafasi ya mwanamke mwenye ulemavu kwani kwa kipindi kirefu wamekua wakipata changamoto bila kuwa na sehemu ya kuziwasilishia.

" Ni kweli Walemavu wanakabiliwa na changamoto kubwa sana lakini wanawake wenye ulemavu changamoto zao ni kubwa zaidi, Kuna ambapo wanafanyiwa ukatili wa kimaumbile lakini hawawezi kujitetea, ni jukumu letu kama Wabunge kuipitisha hoja hii ili iweze kuwepo siku ya wanawake wenye ulemavu.

Niwaombe wabunge kuhakikisha kuwa hoja hiyo itakapoletwa bungeni iwe kwa kuletwa na Mbunge Stella Ikupa mwenyewe au hata Mbunge mwingine basi tuiunge mkono kwa asilimia 100, ili bunge liweze kuridhia, naamini Wabunge mmetuelewa," Amesema Dk Tulia.

Kwa upande wake Mwenyekiti wa Taasisi hiyo ya Ikupa Trust ambaye pia ni Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Katiba na Sheria, Amon Mpanju amewaomba Wabunge hao kuipitisha siku hiyo kwa manufaa ya Watu wenye ulemavu.

“Hii hoja siyo yetu pekee yetu hata wenzetu wa shirika la kimataifa la Un Woman pamoja na shirika la idadi ya watu duniani UNFPA wametuunga mkono katika hili la kuwa na siku hii rasmi," Amesema Mpanju.

Nae Mbunge Stella Ikupa amesema kupitia uwepo wa siku ya mwanamke mwenye ulemavu ni rahisi jamii kubadilisha mtazamo hasi dhidi ya watu wenye ulemavu na kuitumia pia siku hiyo kama sehemu ya kutoa Elimu kwa wananchi dhidi ya vitendo vyenye ukatili.

" Ni ombi langu kwenu Ndugu zetu Wabunge tutakapoileta hoja hii basi iweze kupita, tunaamini kuwa na siku moja Maalum ya wanawake wenye ulemavu kunaweza kusaidia kupunguza vitendo vya ukatili Kwenye jamii yetu," Amesema Stella Ikupa.

Naibu Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dk Tulia Ackson akizungumza katika mkutano wa pamoja baina ya wadau wa watu wenye ulemavu na Wabunge wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania jijini Dodoma.
Mwenyekiti wa Taasisi ya Ikupa Trust na Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Katiba na Sheria, Amon Mpanju akizungumza katika mkutano wa pamoja baina ya wadau wa watu wenye ulemavu na Wabunge ambapo mkutano huo umeandaliwa na Taasisi ya Ikupa Trust jijini Dodoma.
Muandaaji wa Mkutano wa wadau wa watu wenye ulemavu na Wabunge, Mbung wa Viti Maalum, Stella Ikupa akizungumza katika mkutano huo.
Washiriki mbalimbali wakiwemo wadau wa watu wenye ulemavu na Wabunge wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, wakifuatilia mkutano wa pamoja uliowakutanisha ambao umeandaliwa na Mbunge wa Viti Maalum Stella Ikupa kupitia Taasisi ya Ikupa Trust jijini Dodoma.
 

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...