Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam Mhe. Amos Makalla leo amewaonyesha kwa Vitendo Madiwani na Maafisa watendaji Kata namna ya kutatua migogoro inayowasumbua wananchi ambapo ametaka kila mtumishi  kuhakikisha anashughulikia kero za Wananchi.

Mgogoro wa kwanza aliotatua RC Makalla umehusisha Mwanamke mmoja aliedhulumiwa eneo na aliekuwa mchumba wake ambapo inasemekana Mwanaume huyo alitafuta Wakili na kufoji nyaraka za kuonyesha mwanaume huyo ni sehemu ya umiliki na uendelezaji wa eneo hilo ambapo Wakili ametumia Sheria ya Jiji la California nchini Marekani ambapo Mkuu wa Mkoa amekabidhi Jambo hilo kwa Vyombo vya vya dola kwaajili ya kulishughulikia kwa mujibu wa Sheria.

Aidha RC Makalla ametatua Mgogoro wa Mwananchi aliejenga Ukuta na kuziba Barabara za kuingia kwenye makazi ya watu ambapo amemuelekeza Afisa Ardhi Kinondoni kumaliza Mgogoro huo kwa kumuelekeza alieziba Barabara kuvunja na kuachia Barabara.

Pamoja na hayo RC Makalla amewapatia Madiwani na Maafisa watendaji Kata ajenda za kushughulikia ambapo miongoni mwa hizo ni kuimarisha Ulinzi na Usalama wa Wananchi, Usafi endelevu wa Mazingira, Makusanyo ya Mapato na usikilizaji wa kero za Wananchi.

Agenda nyingine alizotoa RC Makalla ni usimamizi wa miradi ya maendeleo, Manispaa kutenga asilimia 10 ya mikopo kwa Vijana, Walemavu na Wanawake pamoja na kujenga umoja na mshikamano wa kazi miongoni mwa Watendaji na kuepuka Migongano na Mivutano.


 

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...