Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Mhe. Amos Makalla leo Juni 08 amefanya Mazungumzo na Kamanda Mpya wa Kanda Maalumu ya Dar es salaam ACP. Jumanne Muliro aliefika kuripoti kwa Mkuu wa Mkoa ambae pia ni Mwenyekiti wa Kamati ya Ulinzi na Usalama baada ya kuteuliwa hivi karibuni na Mkuu wa Jeshi la Polisi IGP, Simon Sirro.

Katika Mazungumzo hayo RC Makalla amemuelekeza Kamanda Muliro kuendelea na Operesheni ya kuwashughulikia kikamilifu Majambazi na wahalifu Jijini humo ili Dar es salaam ibaki kuwa tulivu na Wananchi wafanye shughuli zao Usalama.

Aidha RC Makalla amesema kwa Sasa Hali ya Usalama Dar es salaam ni shwari na hataki kusikia Majambazi yakifanya uhalifu.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...