Kamanda wa Uhifadhi wa Kanda ya Magharibi kutoka Mamlaka  ya ya Usimamizi wa Wanyamapori Tanzania(TAWA) Bigilamungu  Kagoma akionyesha jana bunduki aina ya SMG ilikamatwa hivi karibuni katika doria ya kusaka majangili kwenye mapori ya akiba mbalimbali wakati wa mkutano na waandishi wa habari mjini Tabora.


Kamanda wa Uhifadhi wa Kanda ya Magharibi kutoka Mamlaka  ya ya Usimamizi wa Wanyamapori Tanzania(TAWA) Bigilamungu  Kagoma akionyesha jana meno ya tembo mawili kati ya manne yakamatwa hivi karibuni katika doria ya kusaka majangili kwenye eneo la Wilaya ya Mlele Mkoani Katavi wakati wa mkutano na waandishi wa habari mjini Tabora.


NA TIGANYA VINCENT

MAMLAKA ya ya Usimamizi wa Wanyamapori Tanzania(TAWA) Kanda ya Magharibi imefanikiwa kukamata bunduki za aina mbalimbali 24 na meno ya tembo manne yenye uzito kilo 21.2 katika kipindi cha kuanzia mwezi Aprili hadi Juni mwaka huu.

Taarifa hizo zilitolewa jana mjini Tabora na Kamanda wa Uhifadhi wa Kanda ya Magharibi Bigilamungu Kagoma wakati wa mkutano na waandishi wa habari.

Alitaja aina za bunduki wanalizokamata kuwa ni SMG 1, Riffle 3, Shotgun 1 na gobore 19 ambazo zote hizo zilikuwa zikendesha vitendo vya ujangili katika Mapori mbalimbali ya Kanda ya Magharibi.

Kagoma alisema sanjari na hilo wamefanikiwa kuwakamata watuhumiwa 91 wa makosa mbalimbali yakiwemo ya kuingia hifadhini bila kibali , uwandaji wa wanyamapori, uvuvi haramu na uharibifu wa mazingira.

Kamanda huyo aliongeza kuwa baadhi ya Watuhumiwa wameshafikiwa Mahakamani na wengine wawili walikiri kosa na kulipa faini kwa mujibu wa Sheria ya Uhifadhi.

Aliongeza katika doria hizo pia wamefanikiwa kukamata risasi 38 za bunduki za aina mbalimbali na gololi 76 za gobole ambazo zilikuwa zipangwa kutumiaka katika ujangili katika mapori mbalimbai ya Kanda hiyo.

Kagoma alisema kuwa watumuhimwa wawili kati ya hao walikutwa katika pori la Akiba la Ugalla wakiwa wametoka kuwinda Boko wakiwa na Gobole.

Alitoa kwa wananchi kuendelea kutoa ushirikiano kwa TAWA ili kuwabaini watu wanaoendesha ujangilili na hatamaye waweze kukamatwa na kufikishwa katika vyombo vya Sheria ikiwa ni hatua ya kukomesha vitendo hivyo.

Kagoma alitoa rai kwa Majangili kuachana na vitendo vya kuwinda wanyama na kutafuta shughuli nyingine ya kuwaingizia kipato halali.

Alisema mwananachi ambaye andependa kushirikiana na TAWA katika kuwafichua Majangili kwa Kanda ya Magharibi anaweza kupiga simu namba 0800110048.

Katika hatua nyingine Kagoma alisema wanaendelea na jitihada za kufufua bustani ya wanayama ya Tabora iliyopo jirani na Hospitali ya Kitete kwa ajili kuvutia utalii wa ndani.

Aliwataka wakazi wa Kanda ya Magharibi kujenga utamaduni wa kutemelea vivutio vilivyopo vyawanayapori kwa kuwa gharama kwa Mtanzania ni shilingi 4,000/= kwa siku.

Aidha Kagoma alisema kuwa utaratibu wa kuanza maduka ya nyamapori kwa kanda ya Magharibi bado uko chini na kusema kuwa ni duka mmoja ambalo limeshaanzishwa na liko Katavi.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...