MRATIBU Mkazi wa Umoja wa Mataifa (UN) nchini, Zlatan Milizic, amesema Siku ya Mazingira Duniani ilianzishwa kwa madhumuni ya kuwakutanisha wadau wa mazingira kujadili namna bora ya kuhifadhi mazingira kwa lengo la kukabiliana na mabadiliko ya tabianchi.

Milizic amesema hayo leo June 5,2021 jijini Dodoma wakati wa shughuli ya kilele cha Maadhimisho ya siku ya Mazingira Duniani ambapo amesema Dunia inakabiliwa na hatari ya mabadiliko ya mazingira kutokana na uharibu wa mazingira.

“Changamoto nyingi zinazoikumba dunia kwa sasa ni matokeo ya uharibifu wa ardhi, maji na mazingira.” Ameeleza Milizic.

Hata hivyo amesema UN itasaidia kuharakisha utekelezaji wa mkakati utunzaji mazingira nchini ambao umelenga kuhuisha mfumo ikolojia nchini pamoja na mapitio ya sera ya mazingira

“Shirika litaendelea kuwa mdau wa mstari wa mbele kuwezesha shughuli za utunzaji mazingira nchini na tayari tuna miradi ya kurejesha mifumo ya ikolojia na tutaendelea kushirikiana kukabiliana na changamoto ya taka za plastiki.”Amesema .

Kwa upande wake Mwakilishi Mkazi wa Shirika la Umoja wa Mataifa la Mazingira, (UNEP) Clara Makenya, amesema shirika hilo litaendelea kuwa mdau wa mstari wa mbele kuwezesha shughuli za utunzaji mazingira nchini.

“Tayari tuna miradi ya kurejesha mifumo ya ikolojia na tutaendelea kushirikiana kukabiliana na changamoto ya taka za plastiki.” Clara amesema.
Mratibu Mkazi wa Umoja wa Mataifa nchini, Zlatan Milizic akizungumza na wandishi wa habari katika kilele cha maadhimisho ya siku ya mazingira duniani yaliyofanyika kitaifa leo jijini Dodoma
Mwakilishi Mkazi wa Shirika la Umoja wa Mataifa linaloshughulikia Mazingira UNEP, Clara Makenya akizungumzia maadhimisho ya siku ya mazingira duniani yaliyofanyika kitaifa leo jijini Dodoma

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...