Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Viwanda na Biashara, Dk. Hashil Abadallah akizungumza wakati akifungua warsha ya wadau wa sekta binafsi pamoja na Wizara ya Viwanda na Biashara kujadili mapitio ya rasimu ya Sera ya Maendeleo ya Viwanda Vidogo na Biashara Ndogo leo jijini Dar es Salaam.
Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Viwanda na Biashara, Dk. Hashil Abadallah akisisitiza jambo wakati akifungua warsha ya wadau wa sekta binafsi pamoja na Wizara ya Viwanda na Biashara kujadili mapitio ya rasimu ya Sera ya Maendeleo ya Viwanda Vidogo na Biashara Ndogo leo jijini Dar es Salaam.
Dk. Consolatha Ishebabi (kushoto mbele) kutoka Wizara ya Viwanda na Biashara akiwasilisha rasimu kwa wadau wa sekta binafsi kabla ya kuanza kwa majadiliano kwa washiriki.
Warsha ya wadau wa sekta binafsi pamoja na Wizara ya Viwanda na Biashara kujadili mapitio ya rasimu ya Sera ya Maendeleo ya Viwanda Vidogo na Biashara Ndogo ikiendelea leo jijini Dar es Salaam.
Warsha ya wadau wa sekta binafsi pamoja na Wizara ya Viwanda na Biashara kujadili mapitio ya rasimu ya Sera ya Maendeleo ya Viwanda Vidogo na Biashara Ndogo ikiendelea leo jijini Dar es Salaam.
Mratibu wa Mabaraza ya Kukuza Ujuzi ya Kisekta katika Taasisi ya Sekta Binafsi Tanzania (TPSF), Jane Gonsalues kwenye warsha ya wadau wa sekta binafsi pamoja na Wizara ya Viwanda na Biashara kujadili mapitio ya rasimu ya Sera ya Maendeleo ya Viwanda Vidogo na Biashara Ndogo leo jijini Dar es Salaam.
Washiriki wa warsha ya wadau wa sekta binafsi pamoja na Wizara ya Viwanda na Biashara kujadili mapitio ya rasimu ya Sera ya Maendeleo ya Viwanda Vidogo na Biashara Ndogo wakifuatilia majadiliano leo jijini Dar es Salaam.

WADAU wa sekta binafsi pamoja na Wizara ya Viwanda na Biashara leo wamekutana jijini Dar es Salaam kujadili mapitio ya Sera ya Maendeleo ya Viwanda Vidogo na Biashara Ndogo huku ikiwa ni mchakato wa maboresho wa sera hiyo muhimu nchini.

Akizungumza na wadau hao wakati akizindua mkutano huo, Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Viwanda na Biashara, Dk. Hashil Abadallah amewataka washiriki hao kupitia kwa makini rasimu hiyo na kutoa mapendekezo yatakayoiboresha zaidi ili kupata sera inayokidhi mahitaji na hasa katika dunia ya leo.

Dk. Abdallah amewataka wajumbe waliopata fursa hiyo kuhakikisha wanatoa maoni bila kujipendelea wao pekee, bali kwa kuzingatia maslahi ya wajasiliamali wote.

Aliwataka kutambua kuwa Sera ya Maendeleo ya Viwanda Vidogo na Biashara Ndogo’ nchini inayoandaliwa ibabeba wajasiriamali zaidi ya milioni 4.5 hivyo inaitaji umakini katika maandalizi yake ili kuja na suluhisho ya changamoto nyingi kwa wajasiliamali.

“Kwa bahati nzuri zaidi, sekta hii ndio inayobeba takribani asilimia 98 ya viwanda vyote nchini. Hii ni faraja kwa kuwa malighafi za nchi yetu hasa za wakulima zinapata masoko katika viwanda hivyo hasa ikizingatiwa viwanda vya sekta hii vimesambaa nchini kote na vingi vikijihusisha katika uongezaji thamani hasa wa mazao ya kilimo.” Alisema.

Aidha Naibu Katibu Mkuu alibainisha kuwa Serikali inatambua na kuthamini umuhimu wa sekta binafsi nchini hususan thamani ya uendelezaji wajasiriamali katika kuendeleza shughuli za uchumi wa nchi.

Alisema sera za nchi zimeweka bayana nafasi na jukumu la sekta binafsi katika shughuli za moja kwa moja za uzalishaji na kufanya biashara.

“Dira ya Taifa 2025, Ilani ya CCM ya 2020 -2025 na Mpango wa Tatu wa Miaka Mitano wa Maendeleo, pamoja na mambo mengine zinatilia mkazo kuishirikisha ipasavyo sekta binafsi katika kuendeleza au kukuza jasiriamali katika kukuza biashara zinazochochea mauzo ya nje ili kuleta uwiano wa maendeleo.” Alisema.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...