TIMU ya wataalam wa Jiosayansi kutoka Taasisi ya Jiolojia na Utafiti wa Madini Tanzania (GST) imeanza kufanya uchunguzi Juu ya chanzo cha tope linalobubujika katika mtaa wa Makoka , kata ya Makuburi jijini Dar es Salaam.Wakizungumzia Juu ya kutokea kwa tukio hilo wakazi wa eneo husika wamesema kuwa , hali hii ya kububujika kwa tope unazaidi ya miezi sita sasa na ulianza kidogokidogo ambapo mpaka watu si chini ya sita walitumbukia na kuokolewa na majirani.
Kulingana na Maelezo ya wakazi wa eneo, wamefafanua kuwa hali hii ya kububujika kwa tope inaongezeka sana katika msimu wa mvua hivyo kusababisha barabara hii kupitika Kwa mashaka sana.
Timu ya wataalam wa GST inaendelea kufanya uchunguzi ili kujua nini hasa chanzo cha tope hilo.



Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...