Muhoji amesema hayo katika taarifa aliyoitoa kwa umma kuwa Tume ya Utumishi wa Umma itasikiliza watumishi wa umma na wadau wake wakati wa Maadhimisho ya Wiki ya Utumishi wa Umma yanayoanza kesho Jumatano tarehe 16 hadi 23 Juni, 2021.
“Tume katika maadhimisho ya mwaka huu imeandaa utaratibu ambapo Maafisa wa Tume watapokea na kusikiliza kero na malalamiko ya watumishi wa umma kuhusu masuala mbalimbali ya kiutumishi. Kuanzia Jumatano tarehe 16 hadi 18 Juni, 2021 Maafisa wa Tume watakuwa wilayani Kisarawe, mkoani Pwani na tarehe 21-23 Juni, 2021 watakutana na wadau katika Ofisi ya Tume iliyopo Mtaa wa Luthuli, Jijini Dar es Salaam” amesema Bwana Muhoji.
Muhoji ametoa wito kwa watumishi wa umma na wadau waliopo Kisarawe na Dar es Salaam kufika kwa tarehe hizi mahsusi zilizopangwa ili waweze kuhudumiwa na Maofisa wa Tume kuweza kuzitafutia ufumbuzi changamoto zinazowakabili kiutendaji.
“Watumishi wa
umma na wananchi watakaoshindwa kufika amesema wanaweza kuwasilisha kero na
malalamiko yao kwa kutuma barua pepe kwa anuani ya secretary@psc.go.tz au kupiga simu namba 0738 166
703” amesema.
Kaulimbiu
ya Maadhimisho ya Wiki ya Utumishi wa Umma kwa mwaka 2021 ni: “Kuheshimu tofauti ya nyenzo za kuimarisha
misingi ya utawala wa umma ulio adilifu.”
Kazi kubwa
ya Tume ya Utumishi wa Umma ni kufuatilia na kuhakikisha kuwa Rasilimali Watu
katika Utumishi wa Umma inasimamiwa na kuendeshwa kwa mujibu wa Sheria, Kanuni
na Taratibu.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...