WAZIRI wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Dkt. Dorothy Gwajima, leo amekutana na kufanya mazungumzo na Mkuu wa Mkoa wa Iringa Mhe. Queen Sendiga Kwenye ofisi za Wizara jijini Dodoma.
Viongozi hao wamejadili mwenendo wa utoaji huduma za afya, hali ya watumishi na dawa pamoja na maboresho ya miundombinu kwenye vituo vya kutolea huduma za afya Katika mkoa wa Iringa.
Katika kikao hicho Mkuu wa Mkoa aliambatana na Katibu Tawala wa mkoa Bi. Happynes Seneda.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...