Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu anayeshughulikia masuala ya Sera, Bunge, Uratibu, Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu Mhe. Jenista Mhagama (kulia) akiwa pamoja na Kamishna wa Kazi Brig. Gen. Francis Mbindi wakishiriki mkutano wa 109 wa Nchi Wanachama wa Shirika la Kazi Duniani (ILO) uliofanyika kwa njia ya Mtandao katika Ukumbi wa Mkutano uliopo jengo la PSSSF Jijini Dodoma tarehe 7 Juni, 2021.
Mwenyekiti wa Mkutano huo wa 109 wa Nchi Wanachama wa Shirika la Kazi Duniani Mhe. Omar Zniber akifungua mkutano huo.
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge, Uratibu, Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu) Mhe. Jenista Mhagama akisikiliza mada mbalimbali zilizokuwa zikiwasilishwa katika Mkutano huo wa 109 wa Nchi Wanachama wa Shirika la Kazi Duniani (ILO) uliofanyika kwa njia ya Mtandao.
Baadhi ya Washiriki kutoka Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge, Uratibu, Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu) pamoja na Taasisi zilizopo chini ya Ofisi hiyo wakifuatilia mada mbalimbali zilizokuwa zikiwasilishwa katika Mkutano huo wa 109 wa Nchi Wanachama wa Shirika la Kazi (ILO) uliofanyika kwa njia ya Mtandao katika Ukumbi wa Mkutano uliopo jengo la PSSSF Jijini Dodoma tarehe 7 Juni, 2021.
PICHA ZOTE NA OFISI YA WAZIRI MKUU
(SERA, BUNGE, URATIBU, KAZI, VIJANA, AJIRA NA WENYE ULEMAVU)
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...