Na Amiri Kilagalila,Njombe

Mkuu wa mkoa wa Njombe mhandisi Marwa Rubirya ameagiza kufungwa kwa hoja ambazo zimeonesha ufanisi duni kwenye baadhi ya maeneo katika taarifa ya mdhibiti na mkaguzi mkuu wa serikali CAG wilayani Wanging'ombe licha ya kupata hati safi.

Katika kikao cha baraza maalum la madiwani la kujadili hoja za mdhibiti na mkaguzi mkuu wa hesabu za Serikali Mhandisi Rubirya amemuagiza katibu tawala mkoa wa Njombe Judica Omar kuweka utaratibu mzuri wa kuhakikisha hoja hizo hazijirudii kwenye taarifa ya CAG.

"Katika baadhi ya maeneo kuna hoja zinakuwa zinajirudia,sasa maana yake kuna baadhi ya maeneo kuna ufanisi duni.Tuna jukumu la kuhakikisha tunendelea kuimarisha utendaji kazi wetu ili tuwe na hati nzuri zaidi,Katibu tawala wa mkoa uweke utaratibu ambao utaziwezesha halmashauri zetu kuwajibika ipasavyo ili hoja zote za nyuma kuhakikisha zinafanyiwa kazi"alisema Rubirya

Mkuu wa Wilaya ya Wanging'ombe Lauteri Kanoni amesema kutokana na Halmashauri hiyo kutokuwa na kumbukumbu ya kupata Hari chafu hata mwaka mmoja Hivyo wataendelea kutekeleza maelekezo yanayotolewa Katika kutekeleza miradi ya maendeleo.

"Hesabu zetu nzuri tunazo zitarajia zianzie kwenye kurekebisha dosari ndogo ndogo lakini kwa taarifa nilizonazo halmashauri hii imekuwa ikipata hati safi miaka yote ni matumaini yetu tutaendelea kufanyia kazi hoja ili tusipate dosari"alisema Kanoni

Akisoma taarifa ya ukaguzi wa Hesabu za serikali CAG Bwana  Mulokozi Kishenyi ambaye ni mtunza hazina wa Halmashauri ya Wilaya ya Wanging'ombe amesema halmashauri hiyo imepata hati safi kwa miaka saba mfululizo na hiyo ni kutokana na ushirikiano wa kila upande licha ya kuwapo kwa baadhi ya changamoto zikiwemo upungufu wa watumishi Pamoja na Vitendeakazi yakiwemo Magari.

"Katika ukaguzi wa taarifa za heabu kwa mwaka 2019/2020,halmashauri yetu ilikuwa ina jumala ya hoja 35,hoja 24 sawa na 69% zimefanyiwa kazi kujibiwa pamoja na kufungwa,hoja 8 sawa na 23% utekelezaji wake umefanyika kwa sehemu na hoja 3 sawa na 8% hazijafungwa na zinaendelea kufanyiwa kazi kutokana na sababu mbali mbali kusubiri mamlaka zingine zitekeleze majukumu yake"alisema Mulokozi Kishenyi
 
Ameongeza kuwa "Halmashauri yetu inakabiliwa na upungufu mkubwa wa watumishi kwenye idara ya fedha na biashara na kitengo cha ukaguzi wa ndani ambapo halmashauri ina watumishi 10 wa idara ya fedha kati ya watumishi 125 wanaohitajika"alisema Mulokozi Kishenyi
 
Baadhi ya madiwani akiwemo Geoffrey Nyagawa,Hassan Ngela na Onesmo Lyandala wamesema Ni lazima hatua madhubuti ziwe zinachukuliwa ili kuzifuta hoja hizo ambazo zitaendelea Kuchafua utendaji mzuri wa halmshauri uliopo uliopo.

 

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...