Sekretariet ya Halmashauri Kuu ya Taifa ikiongozwa na Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Daniel Chongolo Jumanne  Julai 6 2021, imeshiriki maadhimisho ya miaka 100 ya kuzaliwa kwa  Chama cha Kikomunisti cha China (CPC)  lilifanyika katika Chuo cha  "Mwalimu Julius Nyerere Leadership School" Kibaha, Mkoa Pwani.

Maadhimisho hayo  yameongozwa na Mhe. Rais wa China  Mhe, Xi Jinping  kwa njia ya mtandao ambapo zaidi ya nchi 50 tofauti zimeshiriki ikiwemo Tanzania ikiwakilishwa na CCM.

Pamoja na Mambo Mengine Ndugu Chongolo ameeleza namna ambavyo Chama Cha CPC kimekuwa na ushirikiano wenye manufa makubwa   sana na CCM. Ushirikiano ambao umezaa matunda na urafiki wa kudumu.

Aidha amesema pamoja na urafiki wa vyama hivi viwili nchi ya China na Tanzania zimeendelea kushirikiana kwa karibu katika mambo mengi ya maendeleo toka mwaka 1963 ikiwemo ujenzi wa reli ya Tazara na kiwanda cha nguo cha Urafiki.

Kaziiendelee
Chamaimara






 

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...