
Mtaalamu wa Sheria Chuo Kikuu cha Dar es Salaam, Galantina Salvatory (kulia) akizungumza na mteja katika Maonesho ya 45 ya Biashara ya Kimataifa katika Viwanja vya Mwalimu Nyerere Jijini Dar es Salaam.
Mshauri na Mnasibu Chuo Kikuu cha Dar es Salaam(UDSM) kurugenzi ya Huduma za Jamii kitengo cha Ushauri na Unasibu Ephraimu Masunga akizungumza na Mwandishi wetu katika Maonesho ya 45 ya Biashara ya Kimataifa yanayoendelea katika viwanja vya Mwalimu Nyerere (SABASABA) Jijini Dar es Salaam.
MSHAURI na Mnasibu kutoka Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (UDSM) Kurugenzi ya Huduma za Jamii Kitengo cha Ushauri na Unasibu, Ephraimu Masunga amesema huduma wanazozitoa zimeleta matokeo mazuri ikiwemo kupandisha viwango vya ufaulu kutokana na wanafunzi wengi kushindwa kufuatilia masomo vizuri wanapopata changamoto mbalimbali.
Akizungumza kwenye maonesho ya Kimataifa ya Biashara (Sabasaba), Masunga amesema wanafunzi wanaopata matatizo wanapaswa kuwaona ili kupata ushauri utakaowasaidia katika masuala ya elimu.
Amesema wanatoa huduma ya ushauri kwenye masuala mbalimbali kama vile uchumi, jamii, elimu, saikolojia na afya.
Amesema wanatoa huduma hizo bure hivyo, watu waende kupata usaidizi wa kisheria na kisaikolojia.
"Migogoro mingi tuliyopokea ni ya kijamii ikiwemo mahusiano, ndoa na elimu. Tunahudumia jumuiya ya wanafunzi na wafanyakazi pamoja na ndugu zao na kadri tunavyoendelea tutapanua huduma." amesema Masunga.
Naye, Mtaalamu wa Sheria, Galantina Salvatory amesema wanatoa msaada wa sheria kwa raia wote na unajikita kwenye kesi za madai.
"Changamoto tunayoipata ni baada ya wateja kuhudumiwa ikiwemo kutolewa hukumu na mteja akishinda hawarudi wanahisi wanaweza kudaiwa fedha. Mwengine akishaharibu kesi hawarudi hivyo wanaonekana hawafanyi kazi kwa ufanisi." amesema.
Pia amesema mwamko sio mzuri licha ya kutoa msaada wa sheria kwa wiki nzima bure.
Amesema watu kutoka nje ndio wengi kuliko waliopo ndani ya chuo, hivyo amewataka kujitokeza kupata usaidizi.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...