WAZIRI wa Afya Maendeleo ya Jamii Jinsia Wazee na Watoto, Dk Dorothy Gwajima amefanya ziara ya kushtukiza katika Hospitali ya Taifa ya Muhimbili kuangalia utekelezaji wa agizo la Rais Samia Suluhu Hassan la wananchi kupata huduma bila kero.

Amesema ziara hiyo pamoja na mambo mengine amefuatilia maagizo ya Rais Samia ikiwemo utaratibu wa kutoa maiti mochwari ambapo zamani watu  walikuwa wanapata tabu sana kuipata miili ya wapendwa wao.

Dk Gwajima anasema wananchi ambao walikua wanaenda kuchukua miili ya wapendwa wao walikua wanadaiwa fedha kwanza lakini katika maelekezo ya Rais Samia alisema uwekwe utaratibu wa maiti kutolewa bila tabu na bila kero.

" Rais Samia alisema uwekwe utaratibu wa maiti kutolewa bila kero kama ni masuala ya kulipa na imebainika Ndugu hawana uwezo basi uwekwe utaratibu mwingine utakaofanya walipe bila kuzuia maiti, nashukuru mmefanyia kazi vizuri eneo hilo ambapo kutokea April hadi Juni mmesajili miili 1,970.

Niwaombe wananchi wote wanaouguza Ndugu tunawaombea wote wapone warudi majumbani, lakini ikitokea mapenzi ya Mungu yametimia wametangulia mbele za haki msiwe na wasiwasi Hospitali zetu zinatekeleza agizo la Rais Samia mwili mtaupata kama mna changamoto ya kifedha mtapewa utaratibu mzuri wa kulipa bili yenu kidogo kidogo," Amesema Dk Gwajima.

Ametoa wito kwa wananchi kutoa ushirikiano kwa wataalamu wote wakiongozwa na Prof Mseru ikiwa ni pamoja nao kufuata utaratibu pindi wanapoenda kuchukua miili ya ndugu zao ili kuepusha usumbufu mdogo mdogo unaojitokeza.

Waziri Dk Gwajima amesema jambo lingine aliloenda kukagua ni kuhusu PF3 ambapo Rais Samia aliagiza Hospitali nchini kuwahudumia wagonjwa wanaopelekwa bila kuangalia PF3 kutoka kituo cha Polisi kwa wale wenye kesi za ajali ama kushambuliwa na kuumizwa.

" Niwapongeze Muhimbili kwa hali mmekua hamrudishi wagonjwa ambao hawana PF3 badala yake mnawahudumia huku utaratibu wa PF3 ukiendelea kushughulikiwa ili taarifa za mgonjwa ziwekwe.

Muhimbili na Hospitali zingine zifanye kama Morogoro Hospitali kwamba Ndugu wa mgonjwa akifika anaunganishwa na mfumo ili wawe wanapata taarifa za mara kwa mara za kuelimishwa jinsi gani wataishi na ndugu hadi akiwa anatoka ili kupunguza kero na changamoto maana tutakua tumeungashwa na ndugu moja kwa moja," Amesema Dk Gwajima.

Dk Gwajima pia ameelekeza kwamba Idara ya Patholojia ni muhimu sana lakini majengo yake yamechoka hivyo wataalamu wa Idara hiyo wanapaswa kukingwa sana.

" Tutateua kikosi kazi kije kuangalia hatma ya Patholojia na idara yake, waseme masuala ya utafiti na miundombinu yaweje na hatma nzima ya idara yenu iweje, mnastahili kupewa uangalizi mzuri," Amesema Dk Gwajima.









 

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...