Wananchi mbalimbali waliojitokeza kwenye maonyesho ya vyuo vikuuu wakipata huduma katika mabanda ya wakala mkubwa wa elimu nje ya nchi Global Education Link (GEL) kwenye viwanja vya Mnazi Mmoja jijini Dar es Salaam.
Wananchi mbalimbali waliojitokeza kwenye maonyesho ya vyuo vikuuu wakipata huduma katika mabanda ya wakala mkubwa wa elimu nje ya nchi Global Education Link (GEL) kwenye viwanja vya Mnazi Mmoja jijini Dar es Salaam.
Wanafunzi wa shule mbalimbali nchini wapata maelezo katika mabanda ya wakala mkubwa wa elimu nje ya nchi Global Education Link (GEL) kwenye maonyesho ya vyuo vikuu yanayoendelea kwenye viwanja vya Mnazi Mmoja jijini Dar es Salaam
Wananchi mbalimbali waliojitokeza kwenye maonyesho ya vyuo vikuuu wakipata huduma katika mabanda ya Global Education Link (GEL) kwenye viwanja vya Mnazi Mmoja jijini Dar es Salaam.
Na Mwandishi Wetu
VYUO Vikuu 10 kutoka nje ya nchi viko nchini kwaajili ya kuelezea fani wanazofundisha na kutafuta ubia na vyuo vya hapa nchini katika utoaji wa elimu ya fani mbalimbali.
Vyuo hivyo nane kutoka nchini India na viwili kutoka Ukraine vimekuja nchini kwa mwamvuli wa wakala wa vyuo vikuu nje ya nchi Global Education Link (GEL), kwaajili ya kushiriki maonyesho ya vyuo vikuu yaliyoandaliwa na Tume ya Vyuo Vikuu (TCU).
Maonyesho hayo ya siku tano yanayoshirikisha vyuo vikuu na taasisi mbalimbali yamenza leo Julai 27,2021 jijini Dar es Salaam katika viwanja vya Mnazi Mmoja na yatanatarajiwa kufunguliwa rasmi kesho Jumanne, Julai 28,2021
Mkurugenzi wa GEL, Abdulmalik Mollel amevitaja vyuo hivyo kuwa ni Chandigarh, Lovely Professional University (LPU), CT, Maharish Makandeshwar, Pandeet Deendayal Energy, Sharda, Rayat Bahra vya India na VN Karazan na Sum State vya Ukraine.
Amesema baadhi ya vyuo vimeahidi kufungua matawi hapa nchini baada ya kuona mahitaji makubwa ya kozi wanazofundisha ambazo wanafunzi wa Tanzania wamekuwa wakizifuata kwenye mataifa yao.
Amesema pia baadhi ya vyuo hivyo vya nje vitaingia makubaliano na vyuo vya hapa nchini kuhusu namna ya kufanyakazi pamoja katika utoaji wa elimu ya juu.
Mollel amesema ujio wa vyuo hivyo ni fursa kwa vyuo vya Tanzania kuangalia namna ya kushirikiana kwenye kozi mbalimbali ikiwemo kubadilishana wanafunzi wanaoendelea na masomo ili kupeana uzoefu.
“Mfano mwanafunzi anaweza kusoma miaka miwili India akaja kumalizia hapa Tanzania na wahapa anaweza kusoma mwaka akamalizia kwenye chuo cha nje, haya ni mambo ambayo vyuo vinapaswa kuangalia namna ya kushirikiana,” alisema Mollel.
Amesema hata vyuo vya nje vinaweza kuitumia fursa hiyo kuangalia kozi ambazo mahitaji yake ni makubwa hapa nchini lakini hazipatikani kwa vyuo vya hapa nchini hivyo kuamua kuweka matawi yake hapa na kuchukua wanafunzi kwenda nchini mwao kusomea kozi hizo.
Mollel amesema ni wakati mwafaka kwa vyuo vya ndani kushirikiana na GEL kutangaza kozi walizonazo ili kuwavutia na kuwaleta wanafunzi kutoka mataifa mbalimbali duniani kusoma kwenye vyuo vyao badala ya kutegemea wanafunzi kutoka nchini pekee.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...