Na Said Mwishehe, Michuzi TV
WAKATI wadau wa mazingira wakiadhimisha Siku ya Mikoko Duniani inayoadhimishwa Julai 26 ya kila mwaka,Msanii maarufu nchini Mrisho Mpoto 'Mjomba Mpoto' amewahamasisha watanzania kuendelea kuhifadhi na kuilinda mikoko iliyopo sambamba na kupanda mingine kwani faida zake ni nyingi.
Akitoa ujumbe wake katika siku ya kuadhimisha Siku ya Mikoko Duniani wakati wadau wa mazingira walipokutana baada ya kukutanishwa na Shirika la Wetlands International , Mpoto amesema ni vema watanzania wakatambua faida za uwepo wa mikoko na kubwa zaidi kushiriki kikamilifu katika kupanda mikoko na iliyopo kuendelea kuitunza kwa kutoikata hovyo.
Amefafanua amejaribu kuangalia katika miaka 1980 na inapozungumziwa delta ya Rufiji ulikuwa ni ukanda uliokuwa na mikoko mingi lakini hivi sasa imendelea kutoweka ingawa Wetlands International kwa kushirikiana na wadau wengine wameendelea kuihifadhi kupitia mikakati mbalimbali.
"Kama mtakumbuka katika ukanda huo wa delta ya Rufiji hata samaki aina ya Uduvi ,dagaa kamba na aina nyingine ya samaki walikuwa wanatokea maeneo yale, leo hii maeneo yamevamiwa na wananchi kwasababu wanakata mikoko kwa ajili ya mahitaji yao yakiwemo ya kilimo, kufanya kuni.
"Lakini ukiangalia ukanda huu wa Afrika Mashariki unaweza kuona jinsi gani ambavyo mikoko iliyoko delta ya Rufiji ni muhimu sana, kwanza ni ya kipekee , mirefu na inamuonekano mzuri imetekekea, lakini ukiangalia kihistoria mikoko ndio kitu pekee kinaweza kuvyonza hewa ukaa ya kaboni hayo lakini sasa hivi wamekwisha kwasababu maeneo yale yamevamiwa na wananchi wanakata mikoko kwaababu kulikuwa na mikoko mingi.
Mpoto wakati anaelezea hatua kwa hatua faida na umuhimu wa miti ya mikoko wadau wa mazingira kutoka kwenye taasisi na mashirika mbalimbali wameonekana kuguswa na jinsi alivyowasilisha ujumbe wake kwa njia ya mashairi ambapo wengi wao wakati wanatoa hotuba zao walikuwa wakimuunga mkono.
Msanii huyo ambaye amejizolea umaarufu mkubwa kwa staili yake ya uimbaji sambamba na mashairi yenye jumbe zinazoeleweka kwa rika zote kwa sasa ameendelea kutumiwa na taasisi binafsi na za umma katika kufanya kampeni mbalimbali kutokana na uwezo alionao wa kufikisha ujumbe kwa njia ya sanaa na jami ikaelewa kwa haraka.
Akizungumza baada ya Mpoto kutoa ujumbe wake kwa njia ya mashairi, mgeni rasmi kwenye maadhimisho hayo Anna Lawuo aliyemwakilisha Kamishna Mhifadhi Misitu wa Wakala wa Huduma za Misitu Tanzania(TFS) Profesa Dos Santos Silayo, amesema Wetlands wametoa mchango mkubwa kwenye kuhifadhi mikoko kupitia programu ambazo wamekuwa wakizisimamia.
Amesisitiza Wetlands International imejitahidi na sasa wamekuja mradi mwingine unaitwa Je, Tupande au tusipande ukiwa unaaminisha ulazima wa kupanda mikoko.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...