NA YEREMIAS NGERANGERA…NAMTUMBO.
Mbunge wa jimbo la Namtumbo Mheshimiwa Vitta Rashidi Kawawa ameyasema hayo katika kikao alichokifanya na wakuu wa idara na vitengo katika ukumbi wa Halmashauri ya wilaya ya Namtumbo kuwa wakulima hawajalalamikia mfumo wa kuuza kwa njia ya stakabadhi ghalani kwa maana hiyo mfumo huo ni mzuri na unafaa kwa wananchi wa wilaya ya Namtumbo.
Kawawa alidai ameanza ziara ya kuzungumza na wananchi wa jimbo lake kusikiliza kero za wananchi lakini alisema katika vijiji alivyozungumza na wananchi inaonyesha wazi wakulima wanafurahishwa na kuuza mazao yao kwa mfumo wa stakabadhi ghalani.
Hata hivyo Kawawa alisema wapo wafanyabiashara wadogo aliowaita kwa jina la wachuzi wanaonesha kutoridhika na mfumo huo kwa kuwa walikuwa wananufaika na mfumo holela wa kuuza mazao lakini aliwaomba wataalamu kusimamia mfumo huo wa kuuza mazao kwa njia ya stakabadhi ghalani kwa lengo la kuwasaidia wananchi waliowengi na wenye kipatao cha chini.
Afisa kilimo,Ushirika na umwagiliaji wa Halmashauri ya wilaya ya Namtumbo Joseph Mbilinyi alimwambia Mbunge huyo kuwa wakulima wa wilaya ya Namtumbo wameuelewa mfumo wa stakabadhi ghalani lakini wanachodai mfumo huo uwekewe bei elekezi na serikali badala ya kuacha wafanyabiashara waamue bei wenyewe hali inayowatia hofu wakulima wa wilaya ya Namtumbo .
Bwana Mbilinyi aliongeza kuwa wananchi wanahoji wakati mfumo wa kuuza mazao kwa mfumo wa stakabadhi ghalani umeanzishwa katika wil;aya ya Namtumbo serikali iliweka bei elekezi na wafanyabiashara walinunua kwa bei ya juu ya ile iliyowekwa na serikali lakini serikali ilipoacha kuweka bei elekezi bei hazieleweki wanadai wakulima alisema bwana mbilinyi.
Mkurugenzi wa Halmashauri ya wilaya ya Namtumbo Evance Nachimbinya kwa niaba ya watumishi wa Halmashauri ya wilaya ya Namtumbo alimpongeza mbunge huyo kwa kufanya kikao na watumishi hao kwa lengo la kujenga ushirikiano katika kutekeleza majukumu ya kuwahudumia wananchi wa Namtumbo.
Nachimbinya alimhakikishia mbunge kuwa wataalamu wa Halmashauri na watumishi wote kwa ujumla wao watampa ushirikiano wa hali na mali Mbunge huyo katika kuhakikisha shughuli za kuwahudumia wananchi wa Namtumbo zinafanikiwa kwa kiwango cha juu.
Jimbo la Namtumbo mkoa wa Ruvuma chini ya mbunge Vitta Rashid Kawawa lina jumla ya kata 21, tarafa 3, vijiji 66 na mamlaka ya miji midogo 2 na miji midogo 7 ambapo wananchi wake ni hodari katika kilimo cha mazao ya biashara na chakula huku ardhi yake ni yenye rutuba na inayofaa kwa kilimo.


Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...