Mkurugenzi Mkuu wa Taasisi ya Taifa ya Utafiti wa Magonjwa ya Binadam (NIMR​), Profesa Yunus Mgaya akizungumza wakati wa ziara ya Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia Profesa Joyce Ndalichako na Mkurugenzi Mkuu wa Tume ya Sayansi na Teknolojia (COSTECH), Dkt. Amosi Nungu katika kituo cha utafiti na maendeleo ya tiba asili (NIMR) Mabibo jijini Dar es Salaam leo Julai 8,2021.
Mkuu wa Kituo cha Tiba Asili Mabibo jijini Dar es Salaam, Dkt. Vitus Nyigo akitoa aelezo juu ya Kituo cha Utafiti na maendeleo ya Tiba Asili Mabibo jijini Dar es Salaa leo wakati wa  ziara ya Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia Profesa Joyce Ndalichako na Mkurugenzi Mkuu wa Tume ya Sayansi na Teknolojia (COSTECH), Dkt. Amosi Nungu katika kituo cha utafiti na maendeleo ya tiba asili (NIMR) Mabibo jijini Dar es Salaam leo Julai 8,2021.
Mkurugenzi Mkuu wa Taasisi ya Taifa ya Utafiti wa Magonjwa ya Binadam (NIMR​), Profesa Yunus Mgaya akizungumza wakati wa ziara ya Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia Profesa Joyce Ndalichako na Mkurugenzi Mkuu wa Tume ya Sayansi na Teknolojia (COSTECH), Dkt. Amosi Nungu katika kituo cha utafiti na maendeleo ya tiba asili (NIMR) Mabibo jijini Dar es Salaam leo Julai 8,2021.
Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia Profesa Joyce Ndalichako na Mkurugenzi Mkuu wa Tume ya Sayansi na Teknolojia (COSTECH), Dkt. Amosi Nungu na Mkurugenzi Mkuu wa Taasisi ya Taifa ya Utafiti wa Magonjwa ya Binadam (NIMR​), Profesa Yunus Mgaya wakiwa katika picha ya pamoja mara baada ya kutembelea kituo cha utafiti na maendeleo ya tiba asili (NIMR) Mabibo jijini Dar es Salaam leo Julai 8,2021.

Na Avila Kakingo, Globu ya jamii
WAZIRI wa Elimu, Sayansi na Teknolojia, Profesa Joyce Ndalichako amewaomba watendaji wa kituo cha Utafiti na Maendeleo ya Tiba Asili (NIMR) kuongeza kasi ya kukamilisha jengo litakalo simikwa mitambo ya kutengeneza dawa za tiba asili hapa nchini.

Ameyasema hayo leo Julai 8,2021 wakati wa ziara ya kutembelea kituo cha tafiti na maendeleo ya tiba asili kilichopo mabibo jijini Dar es Salaam. Amesema kuwa kwa kazi nzuri inayoendelea kufanyika katika kitekeleza mradi huo wa kujenga kituo cha tatifi na maendeleo ya dawa za tiba asili hapa nchini unaonekana na kuendelea kwa kiwango ambacho ni bora zaidi kwani umekidhi vigezo vya urefu na vipimo vinavyotakiwa kulingana na mitambo.

Amesema kuwa ujenzi wa kituo hicho cha utafiti kitaweza kusaidi hata baadae kwani kimezingatia vigezo na hata mitambo mikubwa zaidi inaweza kuja kusimikwa katika kituo hicho.

"Wito wangu kwa NIMR ni shughuli zikamilike mapema kwani fedha zinazohitajika zimeshatolewa na Tume ya Sayansi na Teknoloji (COSTECH)." Amesema Prof.Ndalichako

Hata hivyo Prof.Ndalichako amesema kuwa afya ya binadamu ni kipaumbele kikubwa cha serikali kwani bila usitawi wa mwanamchi hakuna shughuli ya maendeleo inaweza kufanyika ndio maana serikali imekuwa ikiwekeza katika afya ya bianadamu na itaendelea kuwekeza katika sekta hiyo.

"Nidhahiri kuwa serikali itaendelea kuwekeza katika tafiti ambazo zinatatua changamoto ya magonjwa ya binadamu ili kuleta maendeleo katika taifa." Amesema prof.Ndalichako

Kwa upande wa serikali na Tume ya Sayansi na Teknolojia amesema kuwa wataendelea kufanya kazi pamoja kwasababu lengo ni kuhakikisha zile tafiti ambazo zinaleta tija na ustawi wa wananchi ndizo zinazo tiliwa mkazo.

Kwa upande wake Mkurugenzi Mkuu wa Taasisi ya Taifa ya Utafiti wa Magonjwa ya Binadam (NIMR​), Profesa Yunus Mgaya akizungumza wakati wa kuwasilisha taarifa ya utekelezaji wa mradi ukarabati wa jengo la kiwanda kwaajili ya uzalishaji wa dawa mbalimbali za tiba asilia hapa nchini kwa ufadhili wa serikali kupitia tume ya sayansi na Teknolojia (COSTECH) fedha hizo zinaboresha maabara za kutengeneza dawa za tiba asili hapa nchini, na baadhi ya mitambo itakayosimikwa katika maabala hiyo imeshawasili hapa nchini.

Profesa Mgaya amesema kuwa kwa kuzingatia mabadiliko ambayo yalifanyika ya kujenga jengo jipya kwaajili ya kusimika mitambo ya kutengeneza dawa mbalimbali za tiba asilia taasisi hiyo bado haijatumia kiasi cha shilingi milioni 131,324,913 huku imeshatumia kiasi cha milioni 148,675,087.Huku ikitarajia kupokea kiasi kilichobaki cha shilingi milioni 120 (120,000,000) kutoka COSTECH kwaajili ya kukamilisha malengo yake ya awali ya kukamilisha Maabala katika kituo cha utafiti na maendeleo ya tiba asili mabibo jijini Dar es Salaam.

Amesema kuwa licha ya kupokea kiasi cha shilingi milioni 280,000,000 fedha hizo zilitumika kutekeleza mradi huo kwa ukarabati wa maabara za kemia na microbiolojia, kununua kinyonya hewa taka (Fume cupboard), manunuzi ya jokofu ya maabara, manunuzi ya mtambo wa kusafishia maji kwaajili ya kiwanda pamoja na kununulia kifaa cha kupimia sampuli.

Profesa Mgaya amesema kuwa kazi nyingine za kukarabati maabara hiyo ni pamoja na manunuzi na usimikazi wa sakafu aina ya polyfloor na matengenezo ya pembe katika eneo linalotumika sasa kama sehemu ya utafiti na uendelezaji wa dawa.

Ukarabati wa jengo hilo tuaendana na viwango vya uzalishaji ikiwa ni pamoja na kuandaa nyumba ya usindikaji wa dawa na chumba cha majaribio ya muda wa kuishi dawa.

Licha ya hayo Prof. Mgaya ameishukuru serikali kupitia wizara ya afya, maendeleo ya jamii, jinsia, wazee na watoto ambayo iliwekeza katika mitambo ya awamu ya kwanza na miundombinu ya utafiti na uzalishaji wa tiba asili ambapo ilitoa kiasi cha shilingi milioni mia nane(800,000,000) kwa lengo la kununua mitambo ya uzalishaji wa dawa za tiba asili.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...