Na Amiri Kilagalila,Njombe
LICHA ya kuwa halmashauri ya mji wa Njombe imefanya vizuri katika ukusanyaji wa mapato kwa asilimia 136.5 lakini bado kuna maeneo ambayo halmashauri hiyo imekwama katika ukusanyaji wa mapato.

Hayo yamebainishwa katika baraza la madiwani la mwisho wa mwaka lililofanyika July 22 ambapo halmashauri hiyo imevuka malengo katika ukusanyaji wa mapato lakini kuna baadhi ya maeneo ukusanyaji wake umeoneka kuwa ni wa kusua sua.

Wakitoa pongezi kwa halmashauri ya mji Njombe baadhi ya madiwani akiwemo Urlick Msemwa wa kata ya Luponde,Anjela Mwangeni wa viti maalumu na Maichael Uhaula wa Yakobi na Honoratus Mgaya wa Makowo,Wamesema lazima kuongeza jitihada katika suala la mapato ili kuongeza zaidi kiwango cha mapato katika halmashauri hiyo huku wakitazama yale maeneoa mbayo kwa mwaka wa fedha wa 2020/2021 hayakufanikiwa kukusanya mapato kwa ukamilifu na kumuomba mkuu wa Wilaya Njombe Kissa Gwakisa Kasongwa kuwapa Ushirikiano kwani jambo hilo limekuwa na utata kwa muda mrefu.

"Sasa hivi tumejenga soko la kisasa,stendi ya kisasa tungeweza kupata fedha nyingi sana lakini tunakosa kwa kuongeza vistendi vingine barabarani na kuacha stendi kuu lazima tuwe na mshikamano kwenye malengo yetu"alisema Honoratus Mgaya

Mbunge wa jimbo la Njombe Mjini Deo Mwanyika amesema ili mji wa Njombe uweze kukua na kuwa manispaa ni lazima mapato yapatikane ikiwa ni pamoja na mpangilio mzuri wa mji.

"Taarifa nzuri ni nyingi kuliko changamoto hii ni dalili Njema,naona ukusanyaji wa mapato umekuwa mkubwa kwa kuvuka lengo kwa hiyo tunahitaji mshikamano mkubwa sana kwasababu moja ya malengo yetu ni kuwa manispaa.Lazima tuwe na ukusanyaji mzuri wa mapato kwasababu ndio itaonyesha zaidi kweli tunahitaji kuwa manispaa"alisema Mwanyika

Kwa upande wake mkuuwa wilaya ya Njombe Kissa Gwakisa amesema "Kwa mfano swala la soko nilipofika tu mkuu wa mkoa alinieleza nianze kulishughulikia.Tumeshaandaa kamati na namna ya kulishughulikia jambo hili na tutakapo kuwa tayari tutasema nini cha kufanya kikubwa tunaomba ushirikiano na sisi tutakuwa pamoja kuvuka jambo hili ambalo ni changamoto kwa sasa"

Awali akisoma taarifa katika baraza hilo mkurugenzi wa halmashauri ya mji Njombe Iluminata Mwenda amesema kuwa

Halmashauri ya mjiNjombe imefanikiwa kukusanya jumla ya Kiasi cha fedha shilingi Bilioni 4.01 ambayo ni sawa na asilimia 136.5 na kufanya halmashauri kuvuka lengo la asilimia 100.

Kwa upande wa Soko kuu halmashauri ililenga kukusanya fedha kiasi cha milioni 181,900,000 na kufanikiwa kukusanya kiasi cha milioni 93,980,000 huku katika stendi kuu lengo ikiwa ni kukusanya kiasi cha Milioni 440,4000,000 na kufanikiwa kukusanya milioni 390,67800 .

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...