Na.Khadija Seif Michuzi Tv

MKALI wa Muziki wa injili nchini Joel Lwaga amesema anatarajia kufanya tamasha la nyimbo za injili katika nchi mbalimbali ili kutoa burudani na kuupeleka mbele zaidi muziki wa injili.

Tamasha hilo lililopewa jina la "international tour Experience" litafanyika katika nchi mbalimbali huku akiweka wazi kuwa amejiandaa vizuri na ugonjwa wa uviko 19 kwake sio kikwazo.

Akizungumza na Michuzi Tv, llwaga amesema kwa Mwaka huu imekua neema kwake kutokana na Kuanza rasmi tamasha lake la kuzunguka nchi mbalimbali kwa lengo la kutoa Burudani na kuona kwa namna gani Mziki wa injili unafika mbali zaidi.

"Nitaanza nchini Ghana ,Nigeria,Kenya ,Uganda na nchi zingine nyingi lengo ni kuutangaza mziki wetu wa injili ambapo tamasha Hilo litamalizika mwakani mwezi agosti."

Hata hivyo, amesema ametaja Siri inayofanya Mashabiki zake kuupenda Mziki wake hususani rika mbalimbali. “Mashairi yangu ni vitu ambavyo vinanigusa binafsi hivyo navoona watu wanapenda kazi zangu ni wazi kuwa ujumbe Umefika kwa haraka zaidi kutokana na kuguswa kwao na kuguswa mioyo yao kutokana na tungo zangu".

Pia Lwaga amewaahidi Mashabiki zake kuwa hivi karibuni ataachia wimbo mpya aliomshirikisha Msanii kutoka nchi za nje .

"Tour yangu itajumuisha na kufanya video kwa ajili ya baadhi ya kazi zangu ambazo audio tayari nimeshafanya hivyo nnategemea tour hii nitafanya vitu mbalimbali ikiwemo kolabo na Wasanii mbalimbali ambao tayari nimeshazungumza nao."

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...