Katibu Mkuu wa Wizara ya Kilimo, Andrew Wilson Massawe ametembelea na kukagua hatua za mwisho za ujenzi wa Mradi wa Kuongeza Uwezo wa Kuhifadhi Nafaka (Storage Capacity Expansion Project) katika eneo la Babati.
Ujenzi wa mradi huo unatekelezwa na Wakala wa Taifa wa Hifadhi ya Chakula NFRA chini ya Mkandarasi UNIA SP Z O O Kutoka Nchini Poland.
Mradi huo ukikamilika utakuwa na uwezo wa kuhifadhi tani elfu arobaini (40,000).
Katika ziara hiyo Katibu Mkuu Kilimo aliongozana na Afisa Mtendaji Mkuu wa NFRA, Milton Lupa pamoja na baadhi ya wajumbe wa menejimenti ya wakala hiyo.
Mradi huo wa eneo la Babati mpaka sasa umefikia asilimia 99.8 na Katibu Mkuu amefurahishwa na kazi nzuri iliyofanyika na hatua ambayo mradi umefikia.
Aidha ameilekeza Menejimenti ya NFRA kuhakikisha mkandarasi anamalizia kazi zilizobaki ndani ya mwezi mmoja ili Vihenge na Maghala hayo yaweze kuanza kutumika.
Katibu Mkuu Wa Wizara ya Kilimo Andrew Massawe akiwa katika picha ya pamoja na watendaji wa Wakala wa Taifa wa Hifadhi ya Chakula NFRA baada ya kutembelea mradi wa kuongeza uwezo wa kuhifadhi chakula uliopo Babati Mkoa wa Manyara
Katibu Mkuu Wa Wizara ya Kilimo Andrew Massawe akipata maelezo kuhusu mradi wa kuongeza uwezo wa kuhifadhi chakula (storage capacity Expansion Project) kutoka Mhandisi Immani Nzobo. Waliosimama nyuma ni Afisa Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Taifa wa Hifadhi ya Chakula NFRA Milton Lupa na pembeni ni Mkurugenzi wa Masoko Mikalu Mapunda
Katibu Mkuu Wa Wizara ya Kilimo Andrew Massawe akipata maelezo kuhusu mradi wa kuongeza uwezo wa kuhifadhi chakula (storage capacity Expansion Project) kutoka Mhandisi Immani Nzobo (kulia), Katibu Mkuu alitembelea mradi huo ambao umefikia aslimia 99.8 ukiwa na uwezo wa kuhifadhi tani elfu arobaini (40,000)
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...