Na Mwandishi Wetu, Njombe

 Mbolea ya asili inayojulikana na kwa jina Hakika imezinduliwa jana hapa ili kukuza aina ya kilimo kinachoitwa kilimohai (organic farming) kwa ajili ya kupanua soko la mazao yanayotokana na kilimo hicho hasa katika nchi za nje, kuimarisha afya  ya udongo na kuongeza tija katika kilimo cha wanavijiji.

Mbole hiyo inatengenezwa na Kampuni ya Kitanzania ya Guavay na  Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni hiyo, Mhandisi Ahad Katera, ameieleza hafla ya uzinduzi kwamba kwampuni inafanya jitihada ya kuongeza  uzalishaji kutoka tani 3,500 za sasa hadi tani 20,000 kwa mwaka.

“Lengo letu ni kuhakikisha wakulima wa parachichi nchini wanayafikia masoko ya Ulaya na Marekani kwa njia ya  uzalishaji wenye tija na matunda yao kukubarika katika masoko hayo,” amesema.

Bw Katera amefafanua  kuwa  mbolea yao  inalenga  hasa wakulima wa mazao kama parachichi, vanilla, macadamia, cocoa na kahawa na kusema kwamba mazao ya kilimo hai ndiyo yenye soko kimataifa.

Akizindua mbolea hiyo, Mkuu wa Wilaya ya Njombe, Bi.Kisa Kasongwa,  kwa niaba ya Mkuu wa Mkoa, Mhandishi Marwa Rubirya, ameipongeza Kampuni ya Guavay na wadau wote walioshiriki katika utafiti hadi ikapatikana mbolea hiyo ambayo amesema  imethibitishwa kutumika ndani na nje ya nchi.

“Niwapongeze kwa uthubutu huu katika kufanya tafiti kwa kushirikiana na wadau wengine. Ni mfano mzuri kuona kampuni za kitanzania zinawekeza katika sekta muhimu hapa nchini,” amesema Bi.Kasongwa, na kusisitiza uongezaji wa uzalishaji kwani mahitaji ya mbolea nchini ni makubwa.

 “Asilimia 90 ya mbolea inayotumika nchini inaagizwa kutoka nchi za nje, hivyo upatikana wa mbolea hii  utapunguza uagizaji wa mbolea kutoka nje na kuokoa fedha  ya kigeni,” amesema Bi.Kasongwa na kuahidi kwamba serikali itashirikiana na kumpuni hiyo kwani inazalisha mbolea ambayo haina kemikali na kuongeza kwamba ni faraja kwa Tanzania kuwa na mbolea hiyo kwani inafaa kwa vitunguu, mahindi na mpunga.

Amesema parachichi ni zao la mkakati kwa mikoa ya Iringa, Mbeya na Njombe na kwamba mbolea hiyo itainua uzalishaji wa zao hilo na uchumi wa  wakulima.

“Nimefurahi kusikia mmeanza mpango wakufanya tafiti ya mbolea bora zitakazofaa kwa zao la alizeti, ambalo kwa sasa ni kipaumbele cha serikali yetu, katika kupunguza uagizaji wa mafuta  ya kula kutoka nje ya nchi,” amesema

Bi.Kasongwa amewataka maafisa ugani kwenye maeneo ya uzalishaji wa parachichi wawasaidie wakulima kuelewa namna bora ya kutumia  mbolea hiyo, kuandaa mashamba, kulima na kutunza afya ya udongo ili kuongeza tija katika uzalishaji.

Mwakilishi wa Mfadhili mkuu wa utafiti huo kutoka Shirika la Bolnnnovate Afrika, Bi.Shira Mukiibi, amesema utafiti wa mbolea hii utaleta matokeo makubwa katika kuinua kilimo Tanzania na hata nchi jirani.

“Naipongeza Serikali ya Tanzania kwa kuwezesha tafiti mbalimbali za kilimo  kufanyika ambazo zitasaidia kuleta mageuzi kwenye sketa ya kilimo na kuifanya Afrika kujitosheleza kwa chakula,” amesema Bi.Mukiibi

Utafiti wa mbolea hiyo ulianza mwaka 2014 hadi mwaka 2017. Ulishirikisha  taasisi mbalimbali kama Chuo Kikuu Dar es Salaam, Chuo cha Kilimo Cha Sokoine, Chuo Kikuu Cha Makerere, Tume ya Sayansi na Teknolojia na wadau wengine kupitia ufadhili wa Shirika la Bolnnnovate Afrika lenye makao makuu yake, Nairobi Kenya.

Mkuu wa Wilaya ya Njombe Bi.Kisa Kasongwa(watatu kulia) akimkabidhi mfano wa hundi ya milioni moja Mkulima wa Parachichi Bw.Erasto Ngole(wapili kushoto) iliyotolewa na Kampuni ya Guavay wazalishaji wa mbolea ya asili ya Hakika mara baada ya kuzindua mbolea hiyo Mkoani Njombe jana. Wapili kulia ni Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni hiyo, Mhandisi Ahad Katera.
Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya Guavay inayofanya uzalishaji wa mbolea ya asili ya HAKIKA, Mhandisi Ahad Katera akieleza juu mbolea yake katika hafla ya uzinduzi wa mbolea hiyo Mkoani Njombe mara baada ya mbolea hiyo kuthibitishwa kutoka kwa mamlaka husika kuwa inafaa katika kilimo cha parachichi nchini.

 Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya Guavay inayofanya uzalishaji wa mbolea ya asili ya HAKIKA, Mhandisi Ahad Katera(kulia) akizungumza na Mkuu wa Wilaya ya Njombe, Bi.Kisa Kasongwa(kushoto) mara baada ya kufanya uzinduzi wa mbolea hiyo ambayo inafaa kwa kufanya kilimo hali(organic farmer) ambacho mazao yake yanasoko kubwa katika nchi za Ulay.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...