Mbunge wa Jimbo la Dodoma Mjini Mh. Anthony Mavunde amewataka walimu wanawake wa Jiji la Dodoma kuchangamkia fursa za kiuchumi zilizopo Dodoma ili kujiongezea kipato na kujikwamua kiuchumi.
Mbunge Mavunde ameyasema hayo jana wakati wa Hafla ya Walimu Wanawake wa Dodoma “Dodoma Women Teachers Gala” ambapo aliwataka walimu hao kuitumia fursa ya ukuaji wa uchumi wa Jiji la Dodoma kufanya shughuli mbalimbali za kiuchumi kwa kutumia mikopo ya 4% ya mapato ya ndani ya Jiji na Kampuni za ukopeshaji mashine na mitambo mbalimbali.
“Nawapongeza waandaji wa hafla hii ambayo imewakutanisha walimu wanawake kutoka maeneo mbalimbali kuja kujadiliana fursa za kiuchumi na kumkomboa Mwalimu mwanamke kiuchumi,katika hafla ya mwakani tutaifanya kubwa zaidi na kuongeza idadi ya walimu washiriki pamoja na taasisi za kuwajengea uwezo.
Nimefurahi kuona bidhaa za ujasiriamali unaofanywa na walimu,niwaombe walimu wengi zaidi mchangamkie fursa hii iliyopo Dodoma kwa sasa kwa ajili ya kujikwamua kiuchumi na kujiongezea kipato na mimi nipo tayari kuwaunga mkono kufikia malengo yenu hayo”Alisema Mavunde
Akizungumza awali,Mwenyekiti wa WOTE FORUM Mwl. Sheila Chinja amewashukuru walimu wote kwa kujitokeza kwa wingi kushiriki katika hafla hiyo na kuahidi kuiboresha zaidi mwakani ili kuongeza tija katika ukombozi wa kiuchumi wa mwalimu mwanamke.
Hafla hiyo ilihudhuriwa pia na Mwenyekiti wa UWT Mkoa wa Dodma Bi. Neema Majule sambamba na wazungumzaji maarufu nchini Tanzania Bi. Aunt Sadaka * na Bi. Irene Mbowe.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)










Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...